MAMA wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa na mama wa mwigizaji
Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila wamegeuka kituko baada ya
kunaswa wakishangilia kumpata ‘Kanumba mpya’.
Tukio hilo ambalo liliwafanya watu wengi wapigwe na butwaa, lilitokea
hivi karibuni katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo wamama hao
ambao watu hawakudhania kama ni mashosti, walisikika wakipiga shangwe
wakisema wamepata mtoto wa kiume kupitia kwa mtoto wa mama Kanumba
aitwaye Adela kisha kumfananisha na marehemu Kanumba.
Mwandishi wetu
ambaye alikuwepo eneo hilo, alipowauliza kulikoni wapige kelele nyingi
za shangwe, mama Kanumba ndiye alikuwa wa kwanza kuzungumza:
“Tuna furaha sana kuzaliwa kwa Kanumba The Great leo, tulikuwa tukimsubiri kwa hamu sana na hatimaye leo amezaliwa.”
Wakati mama Kanumba alipokuwa akimalizia kuzungumza, mama Lulu naye akadakia:
“Kipindi
chote tulikuwa tukiomba sana tumpate mtoto wa kiume na tulikuwa
tumepanga tumpe jina la Kanumba kwa hivyo hapa tuna furaha kumpata
Kanumba mpya.”
Mama Kanumba na mama Lulu kwa sasa wanadaiwa kuwa ni
marafiki wa kutupwa na mara nyingi wamekuwa wakinaswa katika viwanja
tofauti vya starehe jijini.
No comments:
Post a Comment