POOL PARTY
Saturday, June 22, 2013
JINA LA MTOTO WA KANYE WEST NA KIM LAFAHAMIKA..ANAITWA......
Kwa mujibu wa TMZ mtoto huyo wa kike wa mastaa hao amepewa jina la mwelekeo, yaani namaanisha kama jina la pili la baba yake ni Magharibi ‘West’ sasa yeye anaitwa Kaskazini ‘NORTH’.
Naomba nimtambulishe vizuri, mtoto wa kike wa Kanye West na Kim Kardashian amepewa jina la ‘NORTH WEST’ kwa mujibu wa birth certificate kutoka Cedars-Sinai hospital.
Lakini chanzo kingine kilichokaribu kimeuambia mtandao wa USWeekly kuwa couple hao tayari wamempatia mwanao nickname, atakuwa anaitwa ‘NORI’ kama kifupi cha North.
So Kim mwenye miaka 32 amepata a.k.a nyingine ambayo ni mama ‘North’ au mama ‘Nori’. Haijajulikana bado sababu za Kanye na Kim kuchagua jina la North.
Wewe unalionaje jina la mtoto huyo?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment