MSANII wa filamu aliyeibukia kwenye Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan
‘Jack wa Maisha Plus’ hivi karibuni aliwashangaza watu baada ya kuvaa
kigauni ambacho mara kadhaa alipopozi aliacha wazi sehemu zake nyeti.
Tukio
hilo lilinaswa na paparazi wetu ndani ya Ukumbi wa Sun Ciro,Ubungo
jijini Dar kulikokuwa na uzinduzi wa Shindano la Kigori wa Tanzania
ambapo Jack alikuwa ameongozana na rafiki yake, jina lake
halikufahamika.
Akiwa ukumbini hapo, mwanadashosti huyo aliyeonekana
kula kilevi cha bei mbaya, alikuwa akiwatoa udenda wanaume kutokana na
kigauni chake hicho kifupi hadi wengine kufikia hatua ya kumchana kuwa,
alijichoresha kwa kutovaa ‘kufuli’.
“Huyu naye! Ndo nini sasa kutovaa
kufuli kwenye kadamnasi? Wasanii wetu bwana,” alisikika kijana mmoja
huku Jack akionesha kutojali.
No comments:
Post a Comment