MKALI wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ ametamba kufanya shoo kali ikiwemo kumfunika msanii wa Kenya, Prezzo katika Tamasha la Matumaini 2013 litakalofanyika Sikukuu ya Sabasaba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Diamond ametoa majigambo hayo wakati wa mahojiano na Mtangazaji wa kituo cha Star TV, Sauda Mwilima.
“Nimeahidi kufanya bonge la shoo kwenye Tamasha la Matumaini siku hiyo, mashabiki wangu na wapenzi wa muziki wajitokeze kwa wingi.
“Ninataka kudhihirisha ubora wangu siku hiyo kwa kumfunika vibaya Prezzo,” alisema Diamond.
No comments:
Post a Comment