POOL PARTY

POOL PARTY

Tuesday, June 25, 2013

USHAIDI WA PICHA MME WA JOYCE KIRIA NA VIJANA WENGINE WACHADEMA WAKIWA NA PINGU,KESI YA UGAIDI IGUNGA


Bw.Henry Kilewo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza 

 Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.

Kamanda Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na wtuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013.

POLISI WAMKEMEA JOYCE KIRIA KWA KUANDAMANA, HAYA HAPA NDIO MAJIBU


Inasikitisha kuona kwamba huyu mama Joyce Kiria anaingilia mambo ya kisheria na kutaka kupotosha jamii kwamba hajui mume wake yuko wapi pia nadhani analenga kuichochea jamii kwamba aliyetuhumiwa kutenda uhalifu akikamatwa familia yake iandamane, tendo ambalo pia ni kosa la jinai. Aidha anatakiwa kuheshimu haki za watoto na kuacha kuwatumia katika kinga ya kutetea watu wanaotenda uhalifu (Imetolewa na Advera Senso Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini Tanzania)

 Joyce Kiria akizungumza na waandishi wa habari Jana jijini Dar es salaam ambapo alidai hajui mume wake yuko wapi

"LAZIMA NIFE KABLA YA KUFIKISHA MIAKA 40"...AUNT EZEKIEL

 
WAKATI vifo vikizidi kuwatafuna wasanii, staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel amefunguka na  kudai kuwa hawezi kuishi miaka mingi  na  atakufa mapema kuliko  watu  wanavyodhani.

Aunt Ezekiel alifunguka hayo juzikati alipokuwa  akipiga  stori  na  mwandishi wetu jijini Dar ambapo alibainisha kuwa akijitazama mustakabali wa maisha yake basi anaona kabisa kuwa hawezi kufikisha hata miaka 40  kabla  hajafa.
 

“Daah! Sijielewi kabisa yaani kwa jinsi ambavyo najiona, nikifikisha miaka 40 ni bahati aisee, dunia sasa imebadilika sana,” alisema Aunt.

Monday, June 24, 2013

WASHIRIKI WA BIG BROTHER WAZIDI KUUMBUKA....BINTI MWINGINE ANASWA "AKIJICHUA " BAFUNI


Hali  ni  mbaya  kwa  dada  zetu  walioko  ndani  ya  jumba  la  big  brother  baada  ya  washiriki  wawili  mfululizo  kuanikwa   na  camera  za  jumba  hilo wakipiga  wakipiga  puny**t  bafuni...
 Jana  ilikuwa  ni  zamu  ya  pokello, video  inajieleza
Kuitazama  ni  sharti  uwe  mtu  mzima  na  ni  hiari  pia

BAADA YA OMMY DIMPOZI KUPIGWA NA CHUPA NA MAWE DODOMA ,HATIMAYE AFUNGUKA SOMA ALICHOANDIKA HAPA

 Haya ndio aliyoandika Ommy Dimpoz :

NI ZAMU YA SOGGY DOGGY SASA KUTOLEWA NA CHADEMA


Nguli wa muziki wa kizazi kipya Soggy Doggy Anter aka Anselm Tryphone Ngaiza leo ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, MWAKA 2015.
Msanii huyo ametiririka katika ukurasa wake wa facebook, na hapa nanukuu "Shikamoo Mbunge wa Segerea, Makongoro Mahanga, imetosha sasa nadhani ni zamu yangu kuwatumikia wana-segerea 2015 kupitia CHADEMA" mwisho wa kunukuu. Pia kwenye ukurasa wake wa twitter imesomeka ivyo ivyo.
 
Nilipoongea na Msanii huyu aliniambia ameamua kufanya ivi ili kuwasaidia na kuwaletea maendeleo wana-segerea na watanzania kiujumla.
Pia aliniambia ameamua kugombea kupitia CHADEMA, kwasababu ndo chama kinachoweza kufanya mabadiliko kwenye jamii kwasasa.
Nikamuuliza je amemfuata rafiki yake Joseph Mbilinyi aka "SUGU" katika chama icho, akasema hapana, hawajawahi kupewa ushawishi wowote wa kisiasa na Nguli huyo wa muziki wa Hip Hop.
Wana-Segerea kazi kwenu kijana ameamua na amedhamiria.

JINI KABULA: NAUMWA, NAHISI N’TAKUFA


STAA wa filamu na muziki Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amekiri kuwa katika wakati mgumu kutokana na kukabwa na mashetani usiku na kumsababishia maumivu makali ya mwili hadi kuhisi kufa.

Hivi karibuni Jini Kabula alipotea kwenye ulimwengu wa mastaa jijini Dar hivyo Ijumaa Wikienda likaamua kumtafuta, alipopatikana ndipo likabaini hali yake ni tete kiafya.
Akizungumza na mwanahabari wetu wikiendi iliyopita, Jini Kabula alisema kwa muda mrefu sasa amekuwa mtu wa kuumwaumwa na mwili kukosa nguvu ambapo alishapima vipimo vyote lakini aligundulika kuwa na malaria, akatumia dozi na kuimaliza lakini hali bado siyo nzuri.
Huku akiwa amedhoofu mwili, Jini Kabula alisema kila ikifika usiku wa manane akiwa amelala huwa anakabwa na mtu ambaye hamuoni, hali inayomfanya ashindwe kupumua huku mwili ukikosa nguvu na kuuma kupindukia.

“Nahisi kabisa nakufa kwa jinsi ninavyojisikia mwilini, natamani hata usiku usiingie kwa sababu mateso ninayopata ya kukabwa ni makubwa, wakati mwingine nakesha nikiangalia muvi kwa kuhofia nikilala tu lazima nikabwe.
“Hata rafiki zangu nimeshawaaga na kuwaambia kuwa muda wowote wakisikia nimekufa wasishangae kwa sababu naumwa ila ninayemhurumia ni mwanangu, jamani nitamuacha bado mdogo maskini wa Mungu sijui ni shetani gani ametukumba wasanii,” alisema Jini Kabula kwa masikitiko.

SHAMSA: NAOGOPA SANA NDOA WANAUME NI WATU WA KUBADILIKA, NASUBIRI AHADI YA MUNGU


BAADA ya hivi karibuni mchumba wake anayejulikana kwa jina la Dickson ‘Dick’ kuukacha uchumba, msanii wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford ameibuka na kusema anaogopa sana ndoa.

Akistorisha na paparazi wetu, Shamsa alisema japokuwa mwanamke yeyote anahitaji kuolewa lakini yeye anaogopa kuingia kwenye ndoa kwani wanaume ni watu wa kubadilikabadilika kama kinyonga ambapo huwanyima uhuru wake zao kwa kuwawekea sheria kali.
“Naogopa ndoa mwenzenu, wanaume ni watu wa kubadilikabadilika. Nasubiri ahadi ya Mungu kama ni mapenzi yake nifunge ndoa na Dick basi itakuwa kama siyo siwezi kulazimisha kwani hapendi niigize kitu ambacho siwezi kukiacha,” alisema Shamsa.

PHOTOS:JOYCE KIRIA AKIWA NA WATOTO NA NDUGU ZAKE MTAA WA SAMORA WAKITAKA KUJUA ALIPO MUME WAKE




Mtangazaji wa televisheni ya Chanel 5 EATV Joyce Kiria akiwa amewashikilia watoto wake Lingatone Kileo kulia na Lincorn wakati alipozungumza na waandishi wa habari katika mtaa wa Samora na kupaza sauti kuomba msaada kwa Rais Jakaya Kikwete na watanzania kwa ujumla ili kusaidiwa na kujua aliko mume wake Henry Kileo ambaye inadaiwa amepelekwa Igunga akituhumiwa na kesi huko Joyce Kiria amesema mpaka sasa hajaambiwa kama mume wake yuko wapi hivyo hata kama ana makosa anaomba afahamishwe kwani hajui kinachoendelea mpaka sasa





Joyce Kiria akifafanua mambo mbalimbali mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam huku akiwa amewabeba watoto wake na ndugu zake wengine wakiwa na mambongo yenye ujumbe mbalimbali






Joyce Kiria akendelea kujibu maswali kadhaa ya wanahabari wakati akizungumza nao leo jijini dar es salaam.

Saturday, June 22, 2013

AMANDA APIMA NGOMA, PRESHA YAPANDA YASHUKA



MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alijikuta akipandwa na kushukwa na presha  mara baada ya kwenda hospitali kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi.
Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni, jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari, alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha ikampanda baadaye ikashuka.…

MSANII wa filamu za Kibongo, Tamrina Poshi ‘Amanda’ hivi karibuni alijikuta akipandwa na kushukwa na presha  mara baada ya kwenda hospitali kupimwa Ugonjwa wa Ukimwi.
Kikizungumza na Exclusive chanzo makini ambacho kilishuhudia tukio zima katika Hospitali ya Dokta Mvungi, Kinondoni, jijini Dar kilisema baada ya Amanda kupewa majibu ya vipimo na daktari, alianza kuhaha huku na kule kama mtu aliyechanganyikiwa, kisha presha ikampanda baadaye ikashuka.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Amanda na kumuuliza juu ya tukio hilo ambapo bila hiyana alitiririka:
“Ile ilikuwa ni mara ya tatu kupima ngoma yaani wakati nikisubiri majibu, presha ilipanda ghafla mpaka daktari akawa na wakati mgumu wa kunipa majibu.

“Nilienda kuchukua majibu na sikutaka kuyaangalia, nilimpelekea daktari ambaye aliniambia niko safi yaani sikuamini nilitoka nikiwa naongea peke yangu, nilikuwa sijiamini si unajua tena ujana ni maji ya moto sasa presha ,” alisema Amanda.

IMEVUJA, MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA



TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.

“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.…

Stori: Imelda Mtema
TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Risasi Jumamosi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Risasi Jumamosi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Risasi Jumamosi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

ARNOLD SCHWARZENEGGER NDANI YA 'TERMINATOR' 5

Baada ya kukaa kimya kwa kipindi cha muda mrefu ,muigizaji mkongwe wa filamu maarufu za action Arnold Schwarzenegger, ameamua kurejea upya katika ulingo huo huku 'Terminator 5' ikitegemewa kurekodiwa mwezi January mwaka ujao.

Hii itakuwa ni mara ya 4 kwa mcheza filamu huyo kushiriki katika movie hiyo baada ya kushindwa kushiriki katika Terminator 4 kutokana na majukumu ya u-Governor wa Califolirnia  wakati inatengenezwa
PRO-24

MSANII ATINGA UKUMBINI NA KIVAZI CHA NUSU UCHI HUKU NDANI AKIWA "MTUPU"

MSANII wa filamu aliyeibukia kwenye Shindano la Maisha Plus, Jack Dustan ‘Jack wa Maisha Plus’ hivi karibuni aliwashangaza watu baada ya kuvaa kigauni ambacho mara kadhaa alipopozi aliacha wazi sehemu zake nyeti. 


Jack akiwa kaacha nje nyeti zake (sehemu iliyozibwa).
Tukio hilo lilinaswa na mwandishi  wetu ndani ya Ukumbi wa Sun Ciro, Ubungo jijini Dar kulikokuwa na uzinduzi wa Shindano la Kigori wa Tanzania ambapo Jack alikuwa ameongozana na rafiki yake, jina lake halikufahamika.


Akiwa ukumbini hapo, mwanadashosti huyo aliyeonekana kula kilevi cha bei mbaya, alikuwa akiwatoa udenda wanaume kutokana na kigauni chake hicho kifupi hadi wengine kufikia hatua ya kumchana kuwa, alijichoresha kwa kutovaa ‘kufuli’.



Huyu naye! Ndo nini sasa kutovaa kufuli kwenye kadamnasi? Wasanii wetu bwana,” alisikika kijana mmoja huku Jack akionesha kutojali.

WEMA SEPETU APOTEZA MVUTO....MIKOROGO YAMUATHIRI....MICHIRIZI YAANZA KUPANDA USONI

Matumizi mabaya ya vipodozi yameanza kumuathiri  wema  Sepetu  ambaye  ni  miss Tanzania  2006..
Wema  ambaye umri wake bado  haujamtupa  , hivi  sasa  anakabiriwa na tatizo la  ngozi  kutokana  na michirizi  kusambaa  mwili mzima  hasa  mapajani....

 Kamera  zetu  si  mara  ya  kwanza  kumshuhudia  Mrembo  huyu  akizingirwa  na  uzee  kwani  miezi  kadhaa  nyuma  tuliwahi andika  habari  inayofanana  na  hii  lakini  ikielezea  zaidi  michirizi  ya  mapajani....

Tofauti  na  hivyo, hivi  sasa  michirizi  hiyo   imekimbilia  kifuani  na  mabegani  hali  inayoashiria  kwamba  siku  si  nyingi  itahamia  usoni...

"Ukweli  Wema  Sepetu  sasa  amebaki sura  tu,mwili  umemtupa  kabisa .Nadhani  hii  yote  inatokana  na  matumizi  mabaya  ya  mikorogo"...alisema  shuhuda  mmoja  akimtazama  Wema sepetu  aliyekuwa  jaji  katika  shindano  moja  la  umiss  jijini  Dar



Baada  ya  kumsikia  shuhuda  huyo  akimtoa  kasoro  mrembo  huyo, mwandishi  wetu  alitinga  nyumbani  kwa  Wema  Sepetu  kufanya  naye  mahojiano  juu  ya jambo  hili

Alipofika  nyumbani  hapo, mwandishi  wetu  aligonga  geti  na  kufunguliwa  na  dada  mmoja  ambaye  alidai  kuwa  maadam Wema  alikuwa  amelala  na  kwamba  hawezi  kuamshwa mpaka  aamke  mwenyewe..

PICHA:BOB JUNIOUR AKIPOKEA KICHAPO CHA MWIZI BAADA YA KUIBA




Bob Junior ameshare picha hizi kwenye ukurasa wake wa Facebook na kuandika: Kwa Dizaini hii lazima nirudi kwetu K………..Aaaaah Maisha Haya Ya Bongo?,,,,COMING SOON Huu Mzigo…1 Love.

JINA LA MTOTO WA KANYE WEST NA KIM LAFAHAMIKA..ANAITWA......


Kwa mujibu wa TMZ mtoto huyo wa kike wa mastaa hao amepewa jina la mwelekeo, yaani namaanisha kama jina la pili la baba yake ni Magharibi ‘West’ sasa yeye anaitwa Kaskazini ‘NORTH’.
Naomba nimtambulishe vizuri, mtoto wa kike wa Kanye West na Kim Kardashian amepewa jina la ‘NORTH WEST’ kwa mujibu wa birth certificate kutoka Cedars-Sinai hospital.
Lakini chanzo kingine kilichokaribu kimeuambia mtandao wa USWeekly kuwa couple hao tayari wamempatia mwanao nickname, atakuwa anaitwa ‘NORI’ kama kifupi cha North.
So Kim mwenye miaka 32 amepata a.k.a nyingine ambayo ni mama ‘North’ au mama ‘Nori’. Haijajulikana bado sababu za Kanye na Kim kuchagua jina la North.
Wewe unalionaje jina la mtoto huyo?

Friday, June 21, 2013

DIAMOND PLATNUMZ AKUTANA NA M 2 THE P


Diamond (kushoto) akisalimiana na Mgaza Pembe 'M2 The P'.
...Wakibadilishana mawazo.
Diamond katika pozi na…
Diamond (kushoto) akisalimiana na Mgaza Pembe 'M2 The P'.
...Wakibadilishana mawazo.
Diamond katika pozi na Mgaza Pembe 'M2 The P'.
Msanii mahiri wa Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Nasibu Abdul 'Diamond' juzi Jumatano alikutana na rafiki kipenzi wa marehemu Albert Mangweha, Mgaza Pembe 'M2 The P' katika hoteli ya The Atrium iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam na kubadilishana mawazo. Diamond alikutana na msanii huyo wakati alipokwenda kufanya mahojiano na Sauda Mwilima wa Star TV kuhusu maandalizi ya show yake atakayoifanya kwenye Tamasha la Usiku wa Matumaini litakalofanyika Julai 7 mwaka huu ndani ya Uwanja wa Taifa jijini Dar.

HII NDIO BUSTANI YA MAPENZI YA MULIRO ILIYOPO NCHINI KENYA








Hii ni Bustani iliyopata umaarufu sana huko kwa majirani zetu ...hapo watu bila aibu wanatumia hiyo bustani kama Gesti ....Picha hizi jamaa walitega kamera na kuchukua picha na video za watu tofauti.