POOL PARTY

POOL PARTY

Tuesday, March 18, 2014

Producer Mswaki awajia juu Bongo5 baada ya kuitafsiri project yake kuwa ni Obsession na kutafuta kiki

Kama unakumbuka wiki iliyopita siku ya ijumaa, Mswaki aliongea juu ya project aliyokuwa akitarajia juifanya aliyoipa jina la "Keeping Ngwair Alive" ambapo alikuwa akitarajia kutoa ngoma kadhaa kwa sauti na style ya Ngwea maana anipatia sana, ila alikwamishwa na familia ya Ngwea baada ya kwenda kuwaona na kuomba blessing juu ya swala hilo, ambapo aliambiwa ni mpaka aweke kila kitu kwenye maandishi. Mtandao wa Bongo5 ulitoa makala ikiongelea project hiyo na kuitafsiri kama ni Obbsession na kutafuta kiki tu. Mswaki baada ya kukutana na maandishi hayo, aliamua kutumia ukurasa wake wa Instagram na kusema haya.




Really? #Obsessed#KutafutaKiki#Bongo5 naomba nieleweke hivi... 1.Kwanza kabisa nyie kama chombo cha habari mlikuwa na haki kimsingi ya kunitafuta mimi mwenyewe na kuniuliza kama mlikuwa mnataka kujua kuhusiana na hii project,kuliko KUANDIKA na KUJIPA MAJIBU pasipo kuwa na taarifa za kutosha 2.Mnasema kwamba mimi najaribu au nataka kuchukua character ya marehemu Albert,I CAN NEVER BE ARBERT hata siku moja kwa sababu muziki ni sehemu ndogo sana ya maisha au tabia ya mtu. 

3.Mi naamini kila mtu anaweza kumuenzi marehemu kwa nafasi yake hata kama ni kidogo sana,kama mnanifatilia kwa makini sijawahi kusema kwamba mimi ni ZAIDI ya marehemu Albert. 4.Hiki kitu nilikuwa nakifanya kwa nia njema na nilikuwa naamini ni moja ya njia ya kumfanya Albert aendelee kuishi kimziki kwa upande mwingine. 5.Kuweza kufanya kama marehemu ni moja ya sababu tu iliyonipelekea kufanya#keepingNgweaAliveProject,lakini kimsingi project ilikuwa inamuhusu Ngwea moja kwa moja kuanzia kitu alichokiimba na naamna navyoimba mimi ndo maana nikaenda kuwaona wazazi wake ili nao waweze kupata mwanga wa project nzima. Je kuna wasanii wangapi mashuhuri waliofanya vitu vikubwa sana na wakasahaulika kabisa KIMUZIKI?nilikuwa najaribu kuwa mfano kwa hii project kwa kuleta muamko katika jamii wa kuwambuka watu mashuhuli waliotutangulia KWA CHOCHOTE KIDOGO ULICHONACHO. Ahsante

No comments:

Post a Comment