POOL PARTY

POOL PARTY

Saturday, March 15, 2014

NAZIZI AFA KIMAPENZI NA PRODUCER WA KIBONGO...AACHANA NA MUME WAKE

Hivi karibuni, mmoja wa waasisi wa hip hop nchini Kenya, Nazizi, alithibitisha kuwa ameachana ma mume wake kutoka Tanzania, Vinny, na wapo katika harakati za kupeana talaka Naziz na Vinny wana mtoto mmoja wa kiume. Msanii huyo, ambaye ni member wa kundi la hip hop la Necessary Noize, amekufa kimapenzi na Mtanzania mwingine tena, producer Herry Sappy, anayefanya shughuli zake za kimuziki kwenye studio ya Home Boyz Productions ya Kenya. Kwa mujibu wa bongo5.com, Nazizi amethibitisha kuwa na uhusiano na Herry Sappy tangu Valentine’s Day, Februari 14, na uhusiano wao ni wa dhati Chini hapa ni picha za wapendanao hao, pamoja na moto wa Nazizi na aliyekuwa mume wake.
Nazizi na Herry Sappy wakimbusu mtoto wa rapper huyo
Nazizi na Herry Sappy wakimbusu mtoto wa rapper huyo
Nazizi na aliyekuwa mumewe, Vinny, wakati mapenzi yalipokuwa
Nazizi na aliyekuwa mumewe, Vinny, wakati mapenzi yalipokuwa

No comments:

Post a Comment