Kupitia U HEARDS ya Gossip Cop leo hii, kumekuwa na story ya ugomvi
mkubwa uliotokea usiku wa kuamkia leo katika studio zilizopo Maeneo ya
Leaders, ambapo mastaa wawili ambao wameurudisha uhusiano wao hivi
karibuni "Diamond na Wema" wamejikuta katika ugomvi mkubwa baada ya Ommy
Dimpoz kupost Video inayowaonyesha Diamond, Ommy Dimpoz na Victoria
kimani wakiwa studio,
Ripoti zinadai kuwa Wema alikuja speed katika studio hizo akiongozana na
Aunt Ezekiel, na kuanzisha timbwili akidai kuwa Diamond atakuwa na
uhusiano na Victoria Kimani.
Shuhuda wa blog hii aliekuwepo katika eneo la tukio amesema kuwa ngumi
zilidum kwa takribani masaa mawili huku Producer Tuddy na Ommy Dimpoz
wakihangaika kuachanisha ugomvi huo, Ugomvi huo pia umesababisha Diamond
kushika simu ya Wema na kupasua chini huku wakitupiana maneno machafu
ya wewe umetembea na fula huku mwingine akimwambia na wewe mbona
umetembea na flani na flani, kauli iliyoishia Diamond kumwambia Wema
kuwa yeye ndio anamuweka mjini kwa sasa
Tetesi za kuwepo kwa uhusiano wa kimapenzi kati ya the sexy Victoria
Kimani na Diamond zilianza kuvuma baada ya kuonekana katika pich aya
pamoja wakiwa katika moja ya picha za one project Campaign, ambapo wote
walikan akuwa na uhusiano wa kimapenzi.
No comments:
Post a Comment