Lupita ameyasema hayo alhamisi hii alipohudhuria katika ‘Essence Black Women in Hollywood Luncheon’.
Aliongeza kuwa alikuwa anajionea aibu kiasi cha kushindwa hata kujitazama kwenye kioo, mpaka alipokuja kuanza kupata ujasiri baada ya kumuona super model Alek Wek mwenye ngozi nyeusi akisifiwa na watu kama Oprah kama mwanamke mrembo.
Nyong’o aliongeza kuwa hapo ndipo alipoanza kujifunza kuwa uzuri unakuja kwa mtu yeyote bila kujali rangi ya ngozi yake, hivyo anaamini hiyo pia itawahamasisha wasichana wengine ambao wamekutana na hali kama hiyo.
Lupita alielezea hadithi yake ya utotoni baada ya kupokea barua kutoka kwa binti mdogo aliyemwelezea kuwa anaona Lupita kama mwenye bahati kwa kuwa na mafanikio aliyonayo Hollywood huku akiwa ni ngozi nyeusi. Binti huyo aliendelea kusema kuwa alikuwa anakaribia kuanza mchakato wa kubadili rangi ya ngozi yake mpaka alipoanza kumuona Lupita ambaye ana rangi kama ya kwake na bado amefanikiwa.
“I’m honored to be a symbol of hope to others like the women I used to watch made me feel. I hope my presence on screen leads other little girls on a similar journey [to] feel the validation of your own beauty inside and out.” Alisema Lupita.
No comments:
Post a Comment