POOL PARTY

POOL PARTY

Saturday, July 13, 2013

Chris Brown adai kufuta Graffiti zake kwa upendo wake mwenyewe na si kwa kulazimishwa na Jiji


Chriss brown leo hii ameoneka akitemana na graffiti yake aliyokuwa ameichora kwenye ukuta wa mbele wa nyumba yake iliyoko Hollywood, baada ya kutakiwa kufanya hivyo, na jiji la LA  baada ya majirani kulalamika kuwa hazileti picha nzuri na zinatisha watoto wao.
Ripoti za mwanzo zilikuwa zinadai kuwa CB alikuwa anapingana na jiji la LA  tangu mwezi May kuhusu graffiti hiyo iliyokuwa imechorwa jitu la kutisha (monster), na kupinga kuifuta kwa kudai  kuwa inalindwa na  1st Amendment ya mwaka 1792 inayodai serikali kuheshim mawazo ya aina hiyo
 lakini baada ya kushindwa kwa vita hiyo Brown amesema, ameamua kufuta kwa upendo wake yeye mwenyewe na si kwa kalazimishwa na jiji hilo au kwa  kutishiwa kulipishwa fine kubwa kw akosa hilo
Baada ya majirani kulalamika kuhusu picha hizo, jiji lilimtisha kwa kumpiga fine kubwa kama hataifuta ----leo hii wameonekana wafanyakazi wakipaka rangi nyingine juu ya michoro hiyo.
kwa vyovyote vile, idara ya ujenzi kitengo cha  usalama cha  LA imesema kama wakaguzi wao wataridhika na ufutwaji wa graffiti hiyo, basi CB hatapigwa fine hiyo siku ya kesho.

No comments:

Post a Comment