POOL PARTY

POOL PARTY

Thursday, July 11, 2013

MAMA MZAZI WA PROFESA JAY AGONGWA NA GARI NA KUFARIKI DUNIA....


Picha kushoto ni Profesa J akiwa na mama yake mzazi Bi Rosemary Majanjara Haule enzi za uhai wake...
 
Mama  mzazi  wa  Msanii Profesa Jay  amefariki dunia  usiku  wa  kuamkia  leo  baada  ya  kugongwa  na  gari  maeneo  ya  mbezi  juu  jijini  Dar  alikokuwa  anaishi  na  mwanae.


Habari  zinadai  kwamba, marehemu Bi. Rosemary Manjara  Haule  aligongwa na gari akiwa  anavuka barabara kuelekea  dukani  mida ya saa mbili  na  kwamba  baada  ya  kugongwa  wasamaria  wema walimkimbiza  hospitali  ya  Tumbi  kwa  kutumia  bajaji ambako  mauti  ilimkuta  huko
Profesa  Jay  amethibitisha   hilo  na  kudai  kwamba  ilikuwa  ni  vigumu  sana  kuamini.Mama  yake  alimpigia  simu  na  kumwambia  kuwa  kagongwa  na  gari  na  kwamba  yuko  polisi.Ghafla  simu  yake  ikawa  haipatikani...


Profesa  anasema  kwamba  wakati  anapigiwa  simu  alikuwa  katika  mgahawa  wa  nyumbani  lounge,Namanga Dar  ambako  alikuwa  katika  kikao  na  Lady  jaydee  na  mumewe.

"MAMA ALINIAMBIA MWANANGU NIMEGONGWA NAGARI....NJONI KOPOLISINAANDIKISHA....   MWANANGU NAKUFA....  ALINIAMBIA MAMA NA MARA SIMU IKAKATIKA. KILA NILIPOJARIBU KUPIGA IKAWA HAIPATIKANI..." ALISEMA PROFESA J KWA UCHUNGU. 

Mungu  ailaze  roho  ya  marehemu  mahali  pema  peponi.

No comments:

Post a Comment