Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa osifi za TAMISEMI, jijini Dar, Majaliwa alisema;“Wanafunzi 438, 960…
Naibu Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).Waandishi wa habari wakiwa kazini.
NAIBU Waziri wa Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI
Mhe. Kassim Majaliwa leo ametoa taarifa ya serikali kuhusu wanafunzi
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2015.Akizungumza na wanahabari katika ukumbi wa osifi za TAMISEMI, jijini Dar, Majaliwa alisema;“Wanafunzi 438, 960 kati ya 451,392 waliofaulu mtihani wamechaguliwa kujiunga kidato cha kwanza katika shule za serikali katika awamu ya kwanza.”
Akaongeza: “Idadi hiyo ni sawa na asilimia 97.23 ya wanafunzi waliofaulu mtihani na kwa matokeo hayo yanayonesha kuwa na alama ya juu kabisa kwa wavulana ilikuwa 243 na kwa wasichana 240 kati ya alama 250.”
Aidha, naibu huyo amewaagiza wazazi, walezi, wadau wa elimu na halmashauri zote kukamilisha majengo na kuandaa mazingira ya kuwapokea wanafunzi wote waliochaguliwa kuanza kidato cha kwanza mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment