Waziri Tibaijuka akizungumza na wanahabari.
UMATI wa waandishi wa habari ulifurika leo katika
Ukumbi wa Hotel Hyatt Regency, jijini Dar es Salaam ili kusikiliza ni
nini atazungumza Waziri wa Nyumba na Makazi, Profesa Anna Tibaijuka
ambaye ni mmoja wa watuhumiwa wa sakata la uchotwaji wa fedha za akaunti
ya Tegeta Escrow.
Akizungumza na wanahabari, Profesa Anna alisema: “Sioni sababu ya
kujiuzulu kwa sababu mimi sio mtumishi wa wizara hiyo (Nishati na
Madini), nilichopokea mimi ni msaada wala sijaona kitu kibaya zaidi ya
kufurahia msaada huo ambao unasaidia shule ya watoto kike kama
ninavyoomba na kupewa na watu wadau wengine kama Reginald Mengi.”Kujua
mengi tembelea www.globaltvtz.com
No comments:
Post a Comment