Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha…
Naibu
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia)
akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya
jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na
kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.Mkurugenzi
mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya
UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa
kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania
kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana
uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii
unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha
Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van
Berlekom.Baadhi
ya washiriki wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii
wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi
kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho,
Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji
Tanzania unaoendelea jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu, ArushaUTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.
Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.
Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki zao za msingi.
Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.
Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.
Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.
Alisema kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto.
Mkutano huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
No comments:
Post a Comment