POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, December 17, 2014

Mr Blue kuwekeza katika muziki wake



Nyota wa muziki wa kizazi kipya hasa katika miondoko ya micharazo ambaye pia ni mkurugenzi wa Micharazo Foundation, Mr Blue ameahidi kuutumia mwaka 2015 kwa kuwekeza zaidi katika muziki wake ili aweze kufanya muziki mzuri kwa ajili ya mashabiki na wapenzi wa muziki wake.

Mr. Blue amesema hayo jana jioni wakati akibadilishana mawazo na mwandishi wa Hivisasa blog na kudai kuwa muziki wake mwaka 2014 umemfanya agundue kuwa hakuna msanii anayeweza kulingana naye kama akitulia na kufanya muziki kwa nguvu zake zote.

Mr. Blue anayetamba na video ya wimbo wake ‘Pesa’ amesema kuwa mwaka 2015 utakuwa ni mwaka wake wa kufanya muziki mzuri kwa kuwekeza kwa nguvu zote katika muziki wake ikiwa ni pamoja na kuufikisha katika soko la kimataifa.

No comments:

Post a Comment