Huwezi
kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata
wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo
bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hiiKwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.
Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.
'Uasi mkubwa'
''Msisitizo unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema ''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
'Gharama si mchezo'
Sehemu ya shida ni kuwa upasuaji wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa hivyo unawaalika madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale waliohitimu katika nyanya zingine za utabibu.
Inadaiwa kuwa taratibu zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi moja kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati mgonjwa wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na kuwacha kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.
Juu ya hiyo, iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza urembo bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.
Kwa uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.
'Biashara kubwa'
Lakini labda watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa Korea Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia kisu cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye mahakama.
Malkia aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa upasuaji wa kukuza kifua ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani upasuaji huo ulifanya titi lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.
Analaumu madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ". Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama madawa ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."
Na madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji" Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni juu yako mwenyewe.
No comments:
Post a Comment