Kulia
ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick
Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu
Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa
ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga zawadi za Sikukuu
ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.
Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF
kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo
la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo
katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba
wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine
wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi
kabisa katika mfuko huo.…

kabisa katika mfuko huo.
Mlezi
wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Buloma Foundation kilichopo
Picha ya Ndege Kibaha Bi Simphania Aidan wa kwanza kushoto akipokea
Zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa niaba ya Msimamizi na Mwenye kituo
hicho Bi.Fransisca Kyando Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , wa katikati
ni Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka na wa kwanza kulia ni
Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani.
Watoto wakipokea zawadi za Krismasi kwa Niaba ya wenzao.
Picha
ya pamoja ya Ma Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na watoto pamoja na
Mlezi wao baada ya kupokea zawadi hizo kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi.
Afisa
Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga wa pili
kushoto Erick Chinimbaga akimkabidhi zawadi Mmoja wa walezi wa watoto
hao bwana Revocatus Robert wa kwanza Kulia zawadi za Sikukuu ya
Krismasi kwa Wasichana waliotoka katika Mazingira magumu wanaolelewa na
Kituo cha Agape Mkoani shinyanga, wasichana hao walipata zawadi za
Mafuta, Mbuzi, Mchele, Sabuni,Sukari pamoja na vitu.
Akikabidhi Msaada huo Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri
Mugaka alisema kuwa PSPF inatoa zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watoto
yatima ili nao washerekee vizuri na wasijisikie vibaya , aliongeza kuwa
pamoja na PSPF kuwa na wanachama watu wazima lakini pia inafanya hivyo
kwa watoto ili waanze kuijua PSPF wakiwa wadogo na wakiwa watu wazima
waje kuikumbuka na kujiunga na Mfuko huo Bora wa Pensheni na hata kuja
kufanya kazi katika Mfuko huo.
Nae Afisa Mahusiano wa PSPF kutoka Makao Makuu Coleta Mnyamani
Aliongeza neno kuwa Watoto yatima ni kama watoto wengine ambao
wanahitaji kupata huduma na malezi Bora kama watoto wengine wenye wazazi
au wanaolelewa bila shida yotote, alimalizia kwa kusema kuwa PSPF ipo
pamoja na watoto hao wenye uhitaji na itaendelea kuwasaidia
No comments:
Post a Comment