Na Woinde Shizza, Arusha
MBUNGE wa jimbo la Arumeru Mashariki mkoani Arusha Mhe. Joshua Nassari anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kutuhumiwa na tukio la kumteka mtendaji wa kata ya makiba.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas alisema kuwa Mhe Nassari huyu alikamatwa majira ya saa moja usiku December 16 katika eneo la Doli lililopo katika kijiji…

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Lebaratus Sabas alisema kuwa Mhe Nassari huyu alikamatwa majira ya saa moja usiku December 16 katika eneo la Doli lililopo katika kijiji cha UsaRiver kwenye gari aina ya Land cruiser lenye namba za usajili T 753 AQR.
Alisema kuwa mbunge huyo anatuhumiwa kumteka mtendaji kata aliyefahamika kwa jina la Nemani Ndundu wa kata ya Makiba tarafa ya Mbuguni wilayani Arumeru mkoani Arusha December 15 majira ya saa mbili asubuhi katika eneo la Maji ya Chai.
Kamanda Sabas amesema mtendaji huyo alikumbwa na tukio hilo wakati alipokuwa katika pikipiki yake akielekea kwenye kata ambapo inatuhumiwa kuwa Mh. Nassari alimkamata na kumpiga na kumjeruhi katika sehemu mbalimbali za mwili wake huku akimtaka amuonyeshe majina ya wanachama waliopiga kura katika kituo cha huduma na maendeleo kilichopo katika kata yake.
Kamanda Sabas alisema kuwa mpaka sasa Mhe Joshua Nassari anashikiliwa na polisi na anatarajiwa kufikisha mahakamani ya wilaya ya Arumeru leo December 17 kujibu tuhuma zinazomkabili.

No comments:
Post a Comment