POOL PARTY
Friday, December 19, 2014
BELLA, BABY MADAHA WATINGA GLOBAL TV ONLINE, WAELEZEA WALIVYOJIPANGA KWA SHOO YAO YA BOXING DAY DAR LIVE
Miongoni mwa mambo waliyoeleza ni pamoja na maandalizi ya shoo yao ya Boxing Day itakayofanyika katika Ukumbi wa Burudani wa Dar Live, Mbagala-Zakheem, Dar.
Mastaa hao wamesema wamejipanga kutoa burudani ya kufa mtu siku hiyo na kuwataka mashabiki wao wahudhurie kwa wingi siku hiyo.
Mbali na shoo, pia wamefunguka mambo kibao yakiwemo mahusiano yao, maisha kwa ujumla, projects zao mbalimbali kimuziki na mengineyo.
Video Ya AliKiba Kutoka Leo,Itarushwa Kwenye Vituo Hivi Kwa Mara Ya Kwanza
Video iliyosubiriwa kwa muda mrefu na mashabiki wa Ali Kiba ‘Mwana’itaanza kuonyeshwa ijumaa ya 19 Decemba 2014. Ali Kiba amethibitisha kuwa video imekamilika kwa kutoa kionjo cha video hio na kusema ‘Videoimetayarishwa na muongozaji kutoka Afrika Kusini na imefanyika maeneo ya mjii wa Cape Town” .
Vituo vitakavyo rusha hii video
Cameroon, Ethiopia, Angola, U.S. & U.K. itachezwa kwenye vituo vya 1Musicnetworks.
Nigeria na Ghana itachezwa kwenye kituo cha SOUNDCITYtv.
Uganda itachezwa kwenye kituo cha NTVUganda.
Kenya itachezwa kwenye kituo cha Citizen Tv kwenye kipindi cha Mseto.
Tanzania itachezwa kwenye kituo cha CloudsTV.
MWILI WA AISHA MADINDA WASWALIWA KABLA YA MAZIKO
Mwili wa Aisha Madinda ukiswaliwa kabla ya maziko huko Kigamboni jijini Dar hivi punde.
Mwili wa Aisha Madinda ukiswaliwa kabla ya maziko huko Kigamboni jijini Dar hivi punde.
Ulinzi aliowekewa Diamond kiboko!
Mlinzi kutoka jeshi la Uganda
Hawa askari tuliwaona wakati Diamond Platnumz amewasili Uganda na kupokelewa Airport kwa mbwembwe sana.
Kumbe ulinzi wao uliendelea mpaka siku ya sho ambapo mmoja wao aliwekwa Nje ya chumba cha Diamond na Zari. Ni Mlinzi kutoka jeshi la Uganda akilinda usalama Wa@diamondplatnumz na @zarithebosslady Hii picha akiwa nje ya chumba akiwasubiri wakati wakijiandaa.
DIAMOND, ZARI WAFUNIKA ALL WHITE CIROCPARTY ILIYOFANYIKA KAMPALA UGANDA
Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari' au 'The Boss Lady' akiwekwa sawa kabla ya shoo yake ya All White Ciroc party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Guvnor nchini Uganda.
Staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz' (kulia) akiwa na Zari au 'The Boss Lady' kabla ya kuelekea katika shoo.…
Mfanyabiashara mrembo na muimbaji wa Uganda, Zarinah Hassan 'Zari' au 'The Boss Lady' akiwekwa sawa kabla ya shoo yake ya All White Ciroc party iliyofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Guvnor nchini Uganda.
Subscribe to:
Posts (Atom)