POOL PARTY

POOL PARTY

Monday, December 1, 2014

Ommy Dimpoz kutoa laki 5 kila wiki kwa wiki nne

Naamini utakuwa umeshaiona video mpya ya Ommy Dimpoz "Tupogo Remix" ambayo imetoka leo sio?  sasa Ommy ameamua kutoa laki 5 kila wiki.
 Kuanzia jumatatu ijayo kupitia account zake za mitandao ya kijamii facebook titwer na instagram @ommydimpoz atakua anaendesha shindano la kucheza wimbo huo, shindano alilolipa jina "Lima na Tupogo" ambapo kila mwisho wa wiki mshindi atazawadiwa mtonyo laki 5 cash kutoka mfukoni kwa Ommy dimpoz.
Lima na tupogo ni moja kati ya vionjo kwenye Tupogo, sasa kwasababu mafans wetu wanatuweka hapa na wanatufanya tuwe hapa na wanatupa nguvu ya kufanya kazi zaidi kwahiyo nimeona hii wakati nimetoa hii video ya tupogo, na kama kuwataka radhi hizi kwasababu uanajua tupogo ni video ambayo ingetakiwa kutoka mda mrefu ndio maana nikaamua nifanye remix na niitolee video, ambayo itakuwa ni kama bonus track katika album yangu ambayo itatoka siku ya Valentines.....

Lima na Tupogo ni style ambayo nimewapa nafasi mashabiki wa PKP kutumia nafasi hii kulima lima lima lima, wanakuwa wanalima halafu mshindi kwa kila wiki anaondoka na laki tano na tutakuwa na wiki nne,.....Ili kushiriki kutakuwa na hashtag ya Lima  na Tupogo ambayo tutakuwa tunaweka clip kwenye acc yangu ya instagram facebook na twitter kwahiyo tutakuwa tunafanya kwa kupitia social network kui-promote hiyo Lima na Tupogo na wengine kama wataweza ku-upload youtube

No comments:

Post a Comment