POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, June 19, 2013

KUJITAMBUA; NGUZO MUHIMU KATIKA MAISHA YA UHUSIANO!-2

UAMUZI wako wa kuwa memba wa safu hii ni wa busara sana maana umekuwa mjanja na kila siku utakuwa ukijifunza vitu vipya katika maisha yako ya kimapenzi.

Kuwa na uwezo wa kutambua maana ya uhusiano na thamani yake kunakupa kitu kipya ubongoni mwako na kwa hakika unaendelea kuiva zaidi kwenye ulingo wa mapenzi.


Mada kama inavyosomeka hapo juu, tulianza nayo wiki iliyopita kwa kuona baadhi ya maswali ya wasomaji wangu ambayo yalitupa mwingozo katika mada hii.

Wiki iliyopita tuliona mifano minne lakini leo ili twende sawa, nitachapisha swali moja kati ya yale manne ili kukupa mwanga wa kile kinachojadiliwa katika mada hii.



HEBU TUONE:

Pole na kazi kaka…

UAMUZI wako wa kuwa memba wa safu hii ni wa busara sana maana umekuwa mjanja na kila siku utakuwa ukijifunza vitu vipya katika maisha yako ya kimapenzi.
Kuwa na uwezo wa kutambua maana ya uhusiano na thamani yake kunakupa kitu kipya ubongoni mwako na kwa hakika unaendelea kuiva zaidi kwenye ulingo wa mapenzi.


Mada kama inavyosomeka hapo juu, tulianza nayo wiki iliyopita kwa kuona baadhi ya maswali ya wasomaji wangu ambayo yalitupa mwingozo katika mada hii.
Wiki iliyopita tuliona mifano minne lakini leo ili twende sawa, nitachapisha swali moja kati ya yale manne ili kukupa mwanga wa kile kinachojadiliwa katika mada hii.

HEBU TUONE:
Pole na kazi kaka Joseph. Naitwa (naficha jina lake). Nina mpenzi wangu wa muda mrefu sana, ambaye alinisaidia kunisomesha hadi chuo baada ya baba yangu kufariki. Tatizo huyo jamaa ana mke na amefunga ndoa ya kanisani.
Mimi ni Muislam yeye ni Mkristo. Hivi karibuni amejitokeza mwanaume mwingine ambaye hajaoa na amesema ana lengo la kufunga ndoa na mimi, lakini tatizo yeye ni Mkristo na anataka nibadili dini ili tufunge ndoa.
Yule jamaa wa mwanzo naye hataki kuachana na mimi ingawa ana mke wake na imani yake hairuhusu ndoa ya mke zaidi ya mmoja. Nifanyeje?

PATA FUNZO
Kwanza kabisa tunaona namna ambavyo msichana huyo alianza kufanya makosa kwa kuwa kwenye uhusiano na mume wa mtu. Hakuna malengo unapokuwa kwenye uhusiano na mtu mwenye uhusiano na mwingine.
Ikiwa huyo jamaa ana migogoro kwenye ndoa yake, mtu wa kwanza kulaumiwa ni huyo msichana ambaye kwa muda mrefu amekuwa kwenye uhusiano na mume wa mtu.
Jambo lingine la hatari zaidi, huyo jamaa hana mpango wa kuachana naye, ingawa yupo kwenye ndoa inayomtaka kuwa na mke mmoja tu.
Tatizo jipya linaloonekana sasa ni kwamba, tayari ameshajichanganya na kutaka kuanzisha uhusiano mpya na mwanaume mwingine. Mtego mwingine ni kwamba anatakiwa kubadilisha dini ili aolewe (nilishafafanua hili kwenye mada iliyokuwa na kichwa; Uhusiano wa dini, mila, kabila kwenye uhusiano.

KUJITAMBUA NI KUPI HASA?
Kujitambua ni kujipa thamani, kujikubali na kujipa kipaumbele. Kwanza mwenye kujitambua hawezi kupotezewa muda kwa mtu ambaye ana uhusiano wake.
Utakuwa ukisubiri nini? Kama unategemea amuache wake ili awe na wewe utasubiri sana maana itakuwa ni sawa na fisi anayesubiri mkono wa binadamu udondoke ili aule!
Ukishajipa thamani na kipaumbele hutaruhusu uhusiano usio na malengo katika maisha yako. Utapata muda wa kumchunguza mpenzi wako kabla ya kuuruhusu moyo wako umuingize. Anayejitambua hakurupuki, hutafuta muda wa kutosha wa kumchunguza mtu kabla ya kuingia kwenye uhusiano naye.

BAHATI MBAYA
Kuna baadhi ya watu huamini wakati mwingine huingia kwenye uhusiano kwa bahati mbaya. Hapa hakuna ukweli kabisa. Kila kitu ni namna unavyopanga.
Matokeo ya unavyoishi leo utayaona kesho. Usishangae kila siku unakutana na wanaume waongo ambao wanakuchezea na kukuacha, ukija kushtuka muda umeshakwenda na hakuna anayetaka kukuoa ukadhani ni bahati mbaya!
Rudi nyuma jichunguze, ulikuwa unaishije? Watu walikuwa wanakuchukuliaje? Unajua utakuta mwanaume anatafuta mke wa kuoa kwa muda mrefu sana, lakini hapati.
Kila anayekutana naye ni kicheche tu, anagundua baada ya muda mfupi na kuachana naye. Anajiuliza tatizo liko wapi? Kumbe alisahau kwamba siku za nyuma alikuwa mtu wa kubadilisha wanawake hovyo, kwa hiyo anaowapata ni wale wenye tabia kama zake.
Ndugu zangu, tuachanane na bahati mbaya, kila kitu kizuri hujengewa misingi kabla ya matokeo. Ukiamini hili utafungua ukurasa mpya wa maisha yako.
Kuna watu huwa wanajiuliza, kwa mfano, hivi utajuaje kuwa mtu uliyenaye ana mapenzi ya dhati? Kwa nini watu wanaingia kwenye ndoa na mengine mengi.
Haya tutaona kwa undani zaidi wiki ijayo kwa sababu nafasi yangu ni finyu, USIKOSE!

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers. Ameandikia vitabu vitatu; True Love, Let’s Talk About Love na All
About Love vilivyopo mitaani.

No comments:

Post a Comment