POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, June 19, 2013

GERALD HANDO NUSURA AUAWE

Na Sifae Paul

MTANGAZAJI  mwenye jina kubwa wa Radio Clouds FM, Gerald Hando ‘Mzee Mnoko’  ameponea chupuchupu kuuawa baada ya kutishiwa kwa bastola.

Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilijiri maeneo ya Mwananyamala Kwa Kopa, Dar alfajiri ya Jumatatu wiki hii.

Gerald Hando ‘Mzee Mnoko’ .
Ilikuwaje?

Baada ya kutonywa mkasa huo, gazeti hili liliwasiliana na Hando ambaye siku hiyo alishindwa kutokea kwenye kipindi chake cha Power Breakfast na  alielezea kisa kizima.

Alisema: “Ilikuwa saa 12:40…

Alisema: “Ilikuwa saa 12:40 wakati nakatiza pale Kwa Kopa, kabla sijaingia barabara ya kuelekea Ali Hassan Mwinyi, ghafla lilitokea gari aina ya RAV4. Lilikuwa limebana sana upande wangu, ghafla nikasikia kama limenigonga, niliposhusha kioo, kweli nikaona gari langu limegongwa.
“Nilichungulia kwenye lile gari nikamuuliza dereva kwa ishara vipi?
“Nilipoona hanijibu nilifunga vioo vya gari langu nikawa nimetulia,  nikapigwa na butwaa kumuona yule jamaa ameshuka akiwa na bastola.
“Alinigongea kioo lakini sikufungua, nilikuwa nimetaharuki sielewi nini kinaendelea. Lakini wakati ananitishia kuwa nishuke anipige, kuna mwanamke alikuwa naye kwenye gari lake ambaye alishuka na kumlazimisha warudi kwenye gari lao.
“Akiwa ndani ya gari lake, jamaa alifyatua risasi iliyovunja kioo cha mbele cha gari lake na sijui risasi ilielekea wapi maana nilikuwa nimeshachanganyikiwa.
“Kama hiyo haitoshi, jamaa alishuka kwa mara nyingine akiwa na hasira sana na kunifuata tena akitaka kunifyatulia risasi, alipoona imeshindikana alipasua tairi za kushoto za gari langu huku akiniambia ndiyo mchezo umeanza nitaona.
“Bahati nzuri polisi walishafika eneo la tukio kwa sababu ishu yenyewe ilichukua muda mrefu, tulichukuliwa wote hadi Oysterbay (kituo cha polisi) nikatoa maelezo yangu na kumfungulia jalada la kesi namba OB/RB/10613/13 (SHAMBULIO),” alisimulia Hando.
Hadi tunakwenda mitamboni sakata hilo halikujulikana hatma yake, tunaahidi kuendelea kulifuatilia.

No comments:

Post a Comment