POOL PARTY

POOL PARTY

Saturday, June 22, 2013

IMEVUJA, MIMBA YA PENNY YACHOROPOKA

TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.
Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.

“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.…

Stori: Imelda Mtema
TAARIFA ya ndani zinazodai kwamba, mimba ya mchumba wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nassibu Abdul ‘Diamond’, Peniel Mgilwa ‘Penny’ imechoropoka zimevuja na Risasi Jumamosi imezinasa.

Kwa mujibu wa chanzo makini kilichojitambulisha kwa jina la wifi (jina kapuni) kwa Penny, ni kwamba mtangazaji huyo wa Runinga ya Channel 10 cha jijini Dar hivi sasa  hana ujauzito tena kama wengi wanavyodhani.
“Penny hana mimba jamani, yupo fiti kabisa na sidhani hata kama anatarajia kushika ujauzito leo wala kesho,” kilisema chanzo hicho.

Hata hivyo, wifi huyo alisema kwamba awali kulikuwa na dalili zilizoonesha kwamba Penny alikuwa ni mjamzito kutokana na mtangazaji huyo kutumia vitu vichachu kama vile maembe na mara kwa mara alikuwa akiumwa hadi kufikia kulazwa hospitali.
Inadaiwa kwamba Penny alipotoka hospitali alionekana kuwa fiti zaidi na hakuwa na dalili zozote za kuwa na ujauzito kama ilivyokuwa siku za nyuma.
Baada ya gazeti hili kupata habari hizo lililimpigia simu Penny ili kuthibitisha madai hayo:
Risasi Jumamosi: Mambo vipi, Penny pole sana.
Penny: Pole ya nini sasa?
Risasi Jumamosi: Si nimesikia kwamba unaumwa jamani na ukakumbwa na mkasa mwingine?
Penny: Mkasa gani huo unaousema maana mimi niko fiti tu.
Risasi Jumamosi: Nilisikia kwamba baada ya kuumwa na kulazwa hopsitali mimba yako ikatoka?
Penny: (Kimya kwa dakika 3) Asante ni mipango ya Mungu.
Risasi Jumamosi: Sasa unatarajia lini utapata tena mimba nyingine?
Penny :(Kwachuuuuuu). Simu ilikatwa na hata ilipokuwa ikipigwa tena haikuwa ikipokelewa.

No comments:

Post a Comment