POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, June 21, 2013

AUNTY LULU: MAZISHI YANGU WATAJAA MASHOGA NA WATOTO



MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga pamoja na watoto.
Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye mazishi…
Na Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’ amefunguka kuwa siku akifa anaamini mbali na watu wengine mazishi yake yatatawaliwa na mashoga pamoja na watoto.

Lulu Mathias ‘Aunty Lulu’.
Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Aunty Lulu alisema kutokana na ukweli kwamba wengi wanaompenda na ambao wamemzoea ni watoto waliokuwa wakimsikiliza kwenye Kipindi cha Watoto Shoo kupitia Radio One na ITV na mashoga ambao awali alikuwa kama mama yao, hao ndiyo watakaojaa kwenye mazishi yake.
Alisema sababu kubwa ya msiba wake kujaa mashoga wengi ni kwa kuwa kabla hajabadili mfumo wa maisha anayoishi sasa, alikuwa akiwalea hivyo siku ya mazishi lazima wakumbuke fadhila.
“Unajua kufa ni kama kulala, naamini siku ya mazishi yangu watakaokuwa wengi ni watoto pamoja na mashoga ambao zamani nilikuwa mama yao, wengine ni waandishi na wasanii mbalimbali wa filamu na muziki,”alisema Aunty Lulu.

No comments:

Post a Comment