POOL PARTY

POOL PARTY

Tuesday, October 29, 2013

NEY WA MITEGO AKAIDI AMRI YA BASATA YA KUTOKUVAA MLEGEZO..AWAONYESHA USO WA MBUZI FIESTA


Msanii wa Hip pop Ney wa mitego 'TRUE BOY' Amewaonyesha uso wa mbuzi Basata ambao awali walimwonya kutokana na tabia yake ya kuvaa mlegezo "KATA K" akiwa jukwaani kwa madai ya kuidhalilisha sanaa hiyo..

Katika hali ya kushangaza kabisa Msanii huyo ameonekana kupuuzia agizo hilo la basata na kendelea kuvaa mlegezo wakati akilishambulia Jukwaa huku akishangiliwa na mashabiki lukuki wa Bongo Fleva .


Tukio hilo lilitokea jana wakati wa Show ya FIESTA DAY 2 iliyofanyika kwenye viwanja vya Leaderz Club alipokuwa akiwapagawisha wapenzi wake na kibao chake cha "MUZIKI GANI" Akiwa sambamba na Msanii mwenzake Diamond Platinumz.

Sasa wapenzi wa Bongo fleva wanasubiri Rungu la Basata liweze kufanya kazi yake huku wengi wakionekana kumtetea kwa kudai kuwa kila mtu ana aina ya maisha yake 'Life Style'

No comments:

Post a Comment