POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, March 26, 2014

Diamond aishauri serikali kuzifungia kwanza video na nyimbo kutoka nje ya nchi kwani zina uchafu zaidi kuliko video za wasanii wa hapa Bongo

STAA wa Bongo Fleva Nasseb Abdul’Diamond Platinumz’ amefunguka ameishauri serikali kuzifungia kwanza video na nyimbo kutoka nje ya nchi kwani zina uchafu zaidi kuliko video za hapa Bongo.Kupitia mtandao wa Instagram Diamond aliandika hivi ikiwa kweli tunalengo la kutoipotosha kimaadili jamii yetu na vizazi vyetu pendwa, nafikiri ni vyema tungeanza kuzuia Video na nyimbo za kutoka nje…
Na kuongeza kuwa kuliko kuzuia nyimbo na video za nyumbani ambazo uchafu wake haufikii hata robo ya uliopo kwenye Nyimbo zinazopewa kipaumbele toka nje... Hii ni sawa na kuzidi kuukuza muziki wa nje huku tukiudidimiza na kuua mziki wetu... Will the target of reaching our goals ever be achieved?

No comments:

Post a Comment