POOL PARTY

POOL PARTY

Saturday, June 7, 2014

Hivi Huyu Halima Kimwana ni Nani Kwa Diamond?

Kuna watu wanashangaza kidogo,siyo kwamba tunawafuata majumbani mwao na kugundua tabia zao,kwamba wanakula sana,wachoyo,wachafu au hawapatani na majirani zao,hapana,wanayoyafanya ama kuzungumza,wanatufanya tuwatambue.Lakini tunaishia kuwajua kwa majina na matukio yao.Ukiniuliza babu Tale ni nani,fasta nitakujibu kuwa ni msaidizi wa shughuli za Diamond,Romie Jones nitakuambia ni ndugu yake Diamond,Wema Sepetu,ni usingizi wa Diamond,kwa maana ya mpenzi,lakini ukiniuliza Halima Kimwana ni nani,naweza kulipuuzia swali lako kwa maana sitambui wala kujua ni nani kwa Diamond.
Siwezi kuacha kujiuliza hivi huyu binti wa mjini  ni nani kwa Diamond?rafiki,dada,shemeji yake,mpambe au nani,Au ndiye kiunganishi chake kwa wale viumbe waliosababisha aitwe sukari ya warembo?yeye ni nani haswa hata afikie hatua ya kumchagulia Diamond mpenzi wa kuwa nae,ni nani hasa hata afikie kumaindi uwepo wa Wema kwenye himaya ya Diamond,kajina kake kamezidi kukaa on ea kwa kipindi kirefu kutokana na uwepo wake karibu na Diamond,ana nguvu sana kwa Diamond,Nilipuuzia kwa muda mrefu sana nikiamini ni mtu wake wa karibu wa kumshikia poda awapo lokesheni ya video zake,au anashikilia simu zake awapo stejini,baadae nikadhani kuwa huenda ni msaidizi wa mambo binafsi ya Diamond.Lakini kufikia hatua ya kumpangia Diamond mwanamke  wa kuwa nae,kidogo hapo nashindwa kuelewa,yeye ni nani kwa Diamond?
Wadau mnaojua uhusiano wa huyu dada hebu mtujuze,ni nani,anafanya shuhuli gani,naamini wote mliosoma gazeti hilo mna kiu ya kujua.
Source:Gazeti la KIU ya jibu toleo no 1275 la tarehe 2-5/6/2014 
Via Sintah Blog

No comments:

Post a Comment