Stori: Shakoor Jongo na Musa Mateja
ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu kuripotiwa
kupatanishwa kwa mastaa wawili katika tasnia ya filamu Bongo, Wema
Sepetu na Kajala Masanja, taarifa zisizo na shaka zilizotua kwenye meza
ya Ijumaa Wikienda zinaeleza kwamba upatanisho huo haukusaidia chochote
na sasa bifu jipya limeibuka kati yao.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kilichoomba hifadhi ya jina
lake, zoezi la upatanishi kati ya mastaa hao lililofanyika kwenye msiba
wa dairekta wa filamu za Kibongo, George Tyson, Mbezi Beach jijini Dar
lilikuwa sawa na kazi bure.
“Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa na nia ya dhati ya kumaliza tofauti
zilizokuwepo, walikubali kupatana kwa sababu ya heshima ya waliokuwa
wanawapatanisha lakini kiukweli ilikuwa ni sawa na danganya toto, bifu
limelipuka upya,” kilisema chanzo hicho ambacho ni rafiki wa karibu wa
mastaa hao wakubwa mjini.
TEAM WEMA, TEAM KAJALA WANOGESHA BIFU
Kwa mujibu
wa sosi wetu, ukiachilia mbali kukosekana kwa utayari wa kupatanishwa
kati ya wawili hao, pande mbili za mashabiki wao wenye ushawishi mkubwa
kwenye mitandao ya kijamii waliojipachika majina ya Team Wema na Team
Kajala, zimekuwa zikinogesha bifu hilo kwa kumwagia petroli kwenye moto,
hali inayozidi kutibua mambo.
“Sikia nikwambie, kuna vitu vinafanyika katika mitandao ya kijamii
hasa Instagram kuhusiana na hizi pande mbili halafu wahusika wakuu
wanajifanya hawazijui, kuna Team Wema ambayo inamsapoti Wema na ile ya
Kajala inayoitwa Team Kajala, wenyewe wanawajua fika ni akina nani
wanaounda pande hizo ila ukiwauliza wanajifanya hawajui chochote.
“Wengine wananunuliwa mpaka simu za kisasa zenye uwezo wa kufungua
mitandao ya kijamii ili wasambaze uzushi na uongo kuhusu upande pinzani,
sasa timu hizo ziliposikia juu ya upatanisho huo, ziliwajia juu
wahusika ambapo kila mmoja kwa upande wake alikanusha kupatana na
mwenzake,” kilizidi kutiririka chanzo hicho.
KAJALA HATAKI KABISA SULUHU
Chanzo chetu
kiliendelea kufunguka kuwa Kajala hataki kabisa kusikia kuhusu mambo ya
suluhu kwa sababu Team Wema imemdhalilisha sana mtandaoni kiasi cha
kumpa wakati mgumu kujieleza mbele ya mwanaye, Paula ambaye inadaiwa
naye aliyashuhudia matusi hayo ya nguoni.
“Yaani Kajala anasema labda Wema mwenyewe ndiyo aende kumuomba radhi
kwa kashfa zilizokuwa zinatolewa na timu yake anaweza kumfikiria mara
mbilimbili kuhusu suluhu na siyo kusuluhishwa juujuu tu kama
ilivyotokea,” alizidi kutiririka sosi wetu na kuongeza:
“We si unaona mara ngapi Wema na Kajala wanakutana sehemu na wewe
mwenyewe kama mwandishi unashuhudia, umewahi kuwaona wakiwa pamoja au
hata kusalimiana?”
MSIKIE KAJALA
Baada ya kusikia kauli hizo
kutoka kwa chanzo chetu, kama kawaida ya Ijumaa Wikienda liliingia
mzigoni kutafuta mzani wa habari ambapo wa kwanza kutafutwa alikuwa ni
Kajala ambaye hakutaka kabisa kulizungumzia kwa kina suala hilo. Hebu
msikie:
“Kiukweli mi naona hili tatizo letu linachangiwa na hizi timu ambazo
zipo kwa ajili ya kuongeza matatizo. Nasikia eti baada ya siku ile mimi
na Wema kupatanishwa, watu wa timu yake walimpigia kumuuliza, akakataa
kuwa hajakubali kupatanishwa na mimi ili kuwafurahisha watu wake, sasa
unategemea mimi nitasema nini? Nafikiri siyo rahisi mimi kukaa karibu na
Wema kama zamani,” alisema Kajala.
WEMA NAYE
Kwa upande wa Wema yeye alishangaa
habari hizo na kutoa dukuduku lake kwa kusema anachojua ni kwamba hana
bifu na mtu yeyote, siyo Kajala tu bali mtu yeyote ambaye walikuwa na
tofauti huko nyuma yeye hana bifu naye tena.
“Mi nadhani watu wanahitaji kuona picha ambayo tumepiga pamoja na
Kajala ndiyo waamini kuwa tumemaliza bifu letu, unajua huu unaokuja ni
Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na mimi ni mtoto wa Kiislam sasa nitafungaje
Ramadhan huku nikiwa na bifu na mtu?” alisema Wema.
Kukinzana kwa maelezo ya wawili hao kunatosha kuonesha jinsi ambavyo suluhu ya awali haikuweza kumaliza bifu kati yao.
KUTOKA KWA MHARIRI
Wema na Kajala nyie ni
wasanii wakubwa ambao jamii inawatazama kama kioo chao. Haipendezi
kuendeleza malumbano yasiyo na msingi, huu si wakati wa kuwekeana visasi
bali sameheaneni kutoka ndani ya mioyo yenu na mshirikiane kuisimamisha
sanaa ya filamu za Kibongo.
No comments:
Post a Comment