Na Hamida Hassan
MKALI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa
anasikitika kukosa bwana aliyeahidiwa na marehemu Amina Ngaluma.
Akizungumza na paparazi wetu, Aunt Lulu alisema kabla marehemu Amina
hajapatwa na mauti nchini Thailand, alimuahidi kumtafutia bwana nchini
humo lakini mauti yalimkuta kabla hajamtimizia ahadi hiyo.
“We acha tu, aliniahidi kunitafutia mume baada ya kugundua nasumbuliwa
na wanaume kila wakati lakini ndiyo hivyo tena Mungu akamchukua kabla
hajanitimizia ahadi,” alisema Aunt Lulu.
Amina alifariki mwezi uliopita nchini humo ambapo chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni uvimbe kwenye kichwa.
No comments:
Post a Comment