SAKATA la tuhuma za ubakaji zinazomkabili mume wa Flora Mbasha
sasa limechukua sura mpya baada ya maovu yao mengine kuanikwa
hadharani na ndugu wa Flora…..
Msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cathy ambaye ni dada
binamu wa Flora amedai kuwa kinachowatafuna wawili hao ni
laana waliyoipata kutoka kwa babu wa Flora, marehemu baba
Askofu Moses Kulola…..
Ndugu huyo wa Flora amesema kuwa wawili hao waliwahi kufikia
nyumbani kwa askofu Kulola huko Mwanza,siku chache kabla ya
Kulola kuaga dunia na kufanya madudu mengi ikiwemo kuingiza
askari polisi kwenye chumba cha Kulola.
Ndugu huyo alidai kuwa wawili hao walifikia hatua ya kuingiza
askari kwenye chumba cha askofu Kulola kwa madai ya kuibiwa
sh. 300,000 ( Laki tatu ) za Emmanuel Mbasha, mume wa Flora
huku wakimwaga matusi mazito kwa wajukuu wa Kulola….
“Walifikia pale kwa babu, yule Mbasha akawa na pesa kama laki
tatu hivi, akazihifadhi kwenye nyumba ndogo ya chini
waliyofikia,nyuma ya nyumba ya babu, akawa amesahau alikoziweka
zile pesa basi wakaanza kuwatukana matusi ya nguoni wajukuu wa
babu pale kama hawana akili nzuri, yeye Mbasha na Flora,”
alisema ndugu huyon wa Flora.
Akaendelea kudai kuwa walipoona hakuna ushirikiano kwa wajukuu
wa babu wakaamua kuita polisi waliofika pale nyumbani na
kuanza kufanya upekuzi wa nguvu kwenye kila kona ya nyumba
ya baba Askofu….
“Walipoona hawajafanikiwa kuzipata akaamua kuwaingiza polisi mpaka
chumbani kwa babu, na babu alikuwa hayupo nyumbani, alikuwa
kanisani, sasa aliporudi ndipo alikuta askari chumbani kwake
wakifanya upekuzi. Babu alikasirika sana na kujikuta akimwaga
machozi,” alisema Cathy
Akaendelea kudai kuwa babu alishangaa sana kufikia hatua ya
wawili hao( Flora na mumewe) kutomwamini hata yeye mpaka
kuingiza askari ndani ya chumba anacholala lakini wawili hao
walimpuzaa hata baba Askofu huyo….
“Babu aliwalaani wale na aliwaambia kuwa siku si nyingi maovu
na uchafu wao utajulikana kwenye jamii huko Dar wanakowaibia
watu kwa kujifanya wameokoka wakati siyo kweli na wanatapeli
watu kila siku,akasema wataishia pabaya muda si mrefu,” alisema
Cathy.
Akaendelea kudai kuwa Flora na mumewe hawakuwahi kuomba radhi
kwa babu yao Askofu Kulola mpaka alipofariki, na mpaka leo hii
laana yake bado inaawatafuna sana na haya yanayoendelea ni
matokeo ya laana hiyo.
No comments:
Post a Comment