Kuna watu wanashangaza kidogo,siyo kwamba tunawafuata majumbani mwao na
kugundua tabia zao,kwamba wanakula sana,wachoyo,wachafu au hawapatani na
majirani zao,hapana,wanayoyafanya ama kuzungumza,wanatufanya
tuwatambue.Lakini tunaishia kuwajua kwa majina na matukio yao.Ukiniuliza
babu Tale ni nani,fasta nitakujibu kuwa ni msaidizi wa shughuli za
Diamond,Romie Jones nitakuambia ni ndugu yake Diamond,Wema Sepetu,ni
usingizi wa Diamond,kwa maana ya mpenzi,lakini ukiniuliza Halima Kimwana
ni nani,naweza kulipuuzia swali lako kwa maana sitambui wala kujua ni
nani kwa Diamond.
Siwezi kuacha kujiuliza hivi huyu binti wa mjini ni nani kwa
Diamond?rafiki,dada,shemeji yake,mpambe au nani,Au ndiye kiunganishi
chake kwa wale viumbe waliosababisha aitwe sukari ya warembo?yeye ni
nani haswa hata afikie hatua ya kumchagulia Diamond mpenzi wa kuwa
nae,ni nani hasa hata afikie kumaindi uwepo wa Wema kwenye himaya ya
Diamond,kajina kake kamezidi kukaa on ea kwa kipindi kirefu kutokana na
uwepo wake karibu na Diamond,ana nguvu sana kwa Diamond,Nilipuuzia kwa
muda mrefu sana nikiamini ni mtu wake wa karibu wa kumshikia poda awapo
lokesheni ya video zake,au anashikilia simu zake awapo stejini,baadae
nikadhani kuwa huenda ni msaidizi wa mambo binafsi ya Diamond.Lakini
kufikia hatua ya kumpangia Diamond mwanamke wa kuwa nae,kidogo hapo
nashindwa kuelewa,yeye ni nani kwa Diamond?
Wadau mnaojua uhusiano wa huyu dada hebu mtujuze,ni nani,anafanya
shuhuli gani,naamini wote mliosoma gazeti hilo mna kiu ya kujua.
Source:Gazeti la KIU ya jibu toleo no 1275 la tarehe 2-5/6/2014
Via Sintah Blog
No comments:
Post a Comment