POOL PARTY

POOL PARTY

Thursday, June 19, 2014

Picha: P Square waingiza mzigo mpya wa magari matano ya kifahari

P Square wamenunua magari matano ya kifahari
angalia walichokiandika kwenye mtandao wa Instagram

WizKid ala bata na Tyres na Akon

Star Boy  WizKid anaendelea kula bata na wanamuziki maarufu nchini Marekani, Los Angeles.
Hivi karibuni WizKid alionekana akiwa studio na Chris Brown pamojana Tyga na baadae akiwa na Justin Bieber.
Mwanamuziki / Muigizaji Tyrese alikuwa na house party na alialikwa pamoja na Akon kwenye party hiyo.
WizKid, amepost picha yake akiwa amekaa katikati ya Tyrese na Akon  nakuandika 


“Shoutout Tyrese! Sick house party the other day.”

Monday, June 16, 2014

Instagramers Wamshambulia Diva na Kusema Ameedit Picha zake ili Aonekana na Makalio Makubwa

 
Katika Hali Isiyo ya kawaida kuna baadhi ya watu ama Vikundi Instagram wameanza kumchimba Diva Loveness Baada ya Kujitoa Team Wema, Sasa leo wamekuja na Mpya na Kusema kuwa Diva anajiongezea makalio kwenye picha zake kwa kutumia Photoshop, na Wameenda mbali zaidi na kutoa ushahidi wa baadhi ya Picha jionee mwenyewe hapo chini na Ujudge mwenyewe kama ni kweli ama la kwa kuziangalia hizo Picha:




Angalia hiyo Kabati ya Viatu Ilivyopinda pinda

Angalia Ukuta na Frame ya Mlango ilivyopata Dhahama

Angalia Kiti hapo nyuma na Juu ukuta kwenye rangi ya blue ukuta umeyumba na tako
Wataalamu Kazi Kwenu kutuambia kama ni kweli ama wanamsingizia ..
Khaa Ustaa Kazi Kweli Kweli

Flora Mbasha na Mumewe kumbe wana Laana ya Askofu Kulola

SAKATA  la  tuhuma  za  ubakaji  zinazomkabili  mume  wa  Flora  Mbasha  sasa  limechukua  sura  mpya  baada  ya  maovu  yao  mengine  kuanikwa  hadharani  na  ndugu  wa  Flora…..

Msichana  mmoja  aliyejitambulisha kwa  jina  la Cathy  ambaye  ni  dada  binamu  wa  Flora  amedai  kuwa  kinachowatafuna  wawili  hao  ni  laana  waliyoipata  kutoka  kwa  babu  wa  Flora, marehemu  baba  Askofu  Moses  Kulola…..

Ndugu  huyo  wa  Flora  amesema  kuwa  wawili  hao  waliwahi  kufikia  nyumbani  kwa  askofu  Kulola  huko  Mwanza,siku  chache  kabla  ya  Kulola  kuaga  dunia  na  kufanya  madudu  mengi  ikiwemo  kuingiza  askari  polisi  kwenye  chumba  cha  Kulola.

Ndugu  huyo  alidai  kuwa  wawili  hao  walifikia  hatua  ya  kuingiza  askari  kwenye  chumba  cha  askofu  Kulola  kwa  madai  ya  kuibiwa   sh.  300,000 ( Laki  tatu )    za  Emmanuel  Mbasha, mume  wa  Flora  huku  wakimwaga  matusi  mazito  kwa  wajukuu  wa  Kulola….

“Walifikia  pale  kwa  babu, yule  Mbasha  akawa  na  pesa  kama  laki  tatu  hivi, akazihifadhi  kwenye   nyumba  ndogo  ya  chini  waliyofikia,nyuma  ya  nyumba  ya  babu, akawa  amesahau  alikoziweka  zile  pesa  basi  wakaanza  kuwatukana  matusi  ya  nguoni  wajukuu  wa  babu  pale  kama  hawana  akili  nzuri, yeye  Mbasha  na  Flora,” alisema  ndugu  huyon wa  Flora.

Akaendelea  kudai  kuwa  walipoona  hakuna  ushirikiano  kwa  wajukuu  wa  babu  wakaamua  kuita  polisi  waliofika  pale  nyumbani  na  kuanza  kufanya  upekuzi  wa  nguvu  kwenye  kila  kona  ya  nyumba    ya  baba  Askofu….

“Walipoona hawajafanikiwa kuzipata  akaamua  kuwaingiza  polisi  mpaka  chumbani  kwa  babu,  na  babu  alikuwa  hayupo  nyumbani, alikuwa  kanisani, sasa  aliporudi  ndipo  alikuta  askari  chumbani  kwake  wakifanya  upekuzi. Babu  alikasirika  sana  na  kujikuta  akimwaga  machozi,” alisema  Cathy

Akaendelea  kudai  kuwa  babu  alishangaa  sana  kufikia  hatua  ya  wawili  hao( Flora  na  mumewe)   kutomwamini  hata  yeye  mpaka  kuingiza  askari  ndani  ya  chumba  anacholala  lakini  wawili  hao  walimpuzaa  hata  baba  Askofu  huyo….

“Babu  aliwalaani  wale  na  aliwaambia  kuwa  siku  si  nyingi  maovu   na  uchafu  wao  utajulikana  kwenye  jamii  huko  Dar  wanakowaibia  watu  kwa  kujifanya  wameokoka  wakati  siyo  kweli  na  wanatapeli  watu  kila  siku,akasema  wataishia  pabaya  muda  si  mrefu,” alisema  Cathy.

Akaendelea  kudai  kuwa  Flora  na  mumewe  hawakuwahi  kuomba  radhi  kwa  babu  yao  Askofu  Kulola  mpaka  alipofariki, na  mpaka  leo  hii  laana  yake  bado  inaawatafuna  sana  na  haya  yanayoendelea  ni  matokeo  ya  laana  hiyo.

WEMA Akana Kuwa Mjamzito

Staa wa movie Tanzania a.k.a Mrs. Diamond Platnumz ameamua kuandika ukweli kuhusu stori ulizosikia kwamba kwa sasa ni mjamzito… Kupitia page yake ya instagram Wema ameandika ‘Jamani hizi habari za mimi kuwa pregnant…. sijui watu wanatolea wapi… Im NAT… Dah… I wish I was… But im nat wapenzi wangu’

Picha: Mh. Rais Kikwete alipowaalika Wasanii chakula cha jioni IKULU ndogo Dodoma, #TanzaniaNaiaminia

Mh. Rais Kikwete akiwaalika wasanii kujumuika nae chakula cha jioni IKULU ndogo mjini Dodoma, baada ya kumaliza uzinduzi wa video ya #TUULINDE amabapo ndani yake wameimba wasanii zaidi ya 15....
#TanzaniaNaiaminia
Martin Kadinda, Baby J an Dimpoz
Perfect, Izzo B an Quick....
Uwoya, Shamsha an Johari...
Jb
Shilole an Nuh Mziwanda
Fauzia an G...
Queen Darleen
Wolper...
Wolper an Kajala
Gerald Hando an Ruge Mutahaba...

SUMA MNAZALETI: WASANII BONGO TUNANYONYWA SANA

Msanii anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Suma Mnazaleti ndani ya studio za Global TV Online.
Muongozaji wa kipindi Pamela(kulia) akifanya maojiano na Suma Mnazaleti (kushoto).
Suma kwenye pozi ndani ya Global TV Online.
Na Said Ally    
MSANII anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Suma Mnazaleti, amesema umaskini mkubwa walionao wasanii wa Bongo unatokana na kampuni ambazo zinawadhamini, kwani nyingi zimekuwa zikiwanyonya.
Suma Mnazaleti ambaye kwa sasa anatamba na Wimbo wa Mnazaleti na ule wa Mkatoliki aliomshirikisha  R.O.M.A, ‘alitia timu’ kwenye Ofisi za Global Publishers na kufanya mazungumzo kwenye Kipindi cha Mtu Kati kinachorushwa na Global TV Online.

WEMA, KAJALA BIFU UPYA!

Stori:  Shakoor Jongo na Musa Mateja
ZIKIWA zimepita wiki kadhaa tangu kuripotiwa kupatanishwa kwa mastaa wawili katika tasnia ya filamu Bongo, Wema Sepetu na Kajala Masanja, taarifa zisizo na shaka zilizotua kwenye meza ya Ijumaa Wikienda zinaeleza kwamba upatanisho huo haukusaidia chochote na sasa bifu jipya limeibuka kati yao.
Wema Sepetu akipozi pembeni ya ndinga yake.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha ndani kilichoomba hifadhi ya jina lake, zoezi la upatanishi kati ya mastaa hao lililofanyika kwenye msiba wa dairekta wa filamu za Kibongo, George Tyson, Mbezi Beach jijini Dar lilikuwa sawa na kazi bure.
“Hakuna yeyote kati yao aliyekuwa na nia ya dhati ya kumaliza tofauti zilizokuwepo, walikubali kupatana kwa sababu ya heshima ya waliokuwa wanawapatanisha lakini kiukweli ilikuwa ni sawa na danganya toto, bifu limelipuka upya,” kilisema chanzo hicho ambacho ni rafiki wa karibu wa mastaa hao wakubwa mjini.
TEAM WEMA, TEAM KAJALA WANOGESHA BIFU
Kwa mujibu wa sosi wetu, ukiachilia mbali kukosekana kwa utayari wa kupatanishwa kati ya wawili hao, pande mbili za mashabiki wao wenye ushawishi mkubwa kwenye mitandao ya kijamii waliojipachika majina ya Team Wema na Team Kajala, zimekuwa zikinogesha bifu hilo kwa kumwagia petroli kwenye moto, hali inayozidi kutibua mambo.
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Kajala Masanja.
“Sikia nikwambie, kuna vitu vinafanyika katika mitandao ya kijamii hasa Instagram kuhusiana na hizi pande mbili halafu wahusika wakuu wanajifanya hawazijui, kuna Team Wema ambayo inamsapoti Wema na ile ya Kajala inayoitwa Team Kajala, wenyewe wanawajua fika ni akina nani wanaounda pande hizo ila ukiwauliza wanajifanya hawajui chochote.
“Wengine wananunuliwa mpaka simu za kisasa zenye uwezo wa kufungua mitandao ya kijamii ili wasambaze uzushi na uongo kuhusu upande pinzani, sasa timu hizo ziliposikia juu ya upatanisho huo, ziliwajia juu wahusika ambapo kila mmoja kwa upande wake alikanusha kupatana na mwenzake,” kilizidi kutiririka chanzo hicho.
Mastaa hao wawili wakiwa katika picha ya pamoja.
KAJALA HATAKI KABISA SULUHU
Chanzo chetu kiliendelea kufunguka kuwa Kajala hataki kabisa kusikia kuhusu mambo ya suluhu kwa sababu Team Wema imemdhalilisha sana mtandaoni kiasi cha kumpa wakati mgumu kujieleza mbele ya mwanaye, Paula ambaye inadaiwa naye aliyashuhudia matusi hayo ya nguoni.
“Yaani Kajala anasema labda Wema mwenyewe ndiyo aende kumuomba radhi kwa kashfa zilizokuwa zinatolewa na timu yake anaweza kumfikiria mara mbilimbili kuhusu suluhu na siyo kusuluhishwa juujuu tu kama ilivyotokea,” alizidi kutiririka sosi wetu na kuongeza:
“We si unaona mara ngapi Wema na Kajala wanakutana sehemu na wewe mwenyewe kama mwandishi unashuhudia, umewahi kuwaona wakiwa pamoja au hata kusalimiana?”
MSIKIE KAJALA
Baada ya kusikia  kauli hizo kutoka kwa chanzo chetu, kama kawaida ya Ijumaa Wikienda liliingia mzigoni kutafuta mzani wa habari ambapo wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Kajala ambaye hakutaka kabisa kulizungumzia kwa kina suala hilo. Hebu msikie:
“Kiukweli mi naona hili tatizo letu linachangiwa na hizi timu ambazo zipo kwa ajili ya kuongeza matatizo. Nasikia eti baada ya siku ile mimi na Wema kupatanishwa, watu wa timu yake walimpigia kumuuliza, akakataa kuwa hajakubali kupatanishwa na mimi ili kuwafurahisha watu wake, sasa unategemea mimi nitasema nini? Nafikiri siyo rahisi mimi kukaa karibu na Wema kama zamani,” alisema Kajala.
WEMA NAYE
Kwa upande wa Wema yeye alishangaa habari hizo na kutoa dukuduku lake kwa kusema anachojua ni kwamba hana bifu na mtu yeyote, siyo Kajala tu bali mtu yeyote ambaye walikuwa na tofauti huko nyuma yeye hana bifu naye tena.
“Mi nadhani watu wanahitaji kuona picha ambayo tumepiga pamoja na Kajala ndiyo waamini kuwa tumemaliza bifu letu, unajua huu unaokuja ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhan na mimi ni mtoto wa Kiislam sasa nitafungaje Ramadhan huku nikiwa na bifu na mtu?” alisema Wema.
Kukinzana kwa maelezo ya wawili hao kunatosha kuonesha jinsi ambavyo suluhu ya awali haikuweza kumaliza bifu kati yao.
KUTOKA KWA MHARIRI
Wema na Kajala nyie ni wasanii wakubwa ambao jamii inawatazama kama kioo chao. Haipendezi kuendeleza malumbano yasiyo na msingi, huu si wakati wa kuwekeana visasi bali sameheaneni kutoka ndani ya mioyo yenu na mshirikiane kuisimamisha sanaa ya filamu za Kibongo.

Saturday, June 14, 2014

TAMASHA LA KUZINDUA VIDEO YA MUUNGANO LAFANA MJINI DODOMA

Msanii wa mziki alietokea EBSS, Menina na Rachael Kizunguzungu wakifatilia uzinduzi wa
Mwanamziki wa Twanga Pepeta, Kalala Junior (katikati).
Umati wa watu waliojitokeza katika uzinduzi wa Video ya Wimbo wa Muungano katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Reharsal ya Mwisho kwa wasanii katika uwanja wa jamhuri hapa Dodoma masaa machache kabla ile show kubwa. #Tanzania Naiaminia

 
wasanii wakielekea katika jukwaa kuu.

Kwa Mara ya Kwanza Baada ya Muda Mrefu Jack Wolper Anaswa Live Live Ndani ya Malavidavi

Stori: shakoor jongo
KABANG! Baada ya kutoonekana katika pozi za kimahaba kwa muda mrefu, kwa mara ya kwanza, staa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe ‘Gambe’ amenaswa ‘live’ na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu, Risasi Jumamosi limesheheni.
Kwa muda mrefu Wolper amekuwa makini na picha zake za kimahaba tangu alipokuwa akitoka kimapenzi na mfanyabiashara maarufu jijini Dar, Abdallah Mtoro ‘Dallas’.
CHANZO CHAMWAGA MTONYO
Awali, chanzo makini kilipenyeza habari kuwa kuna mawasiliano yamenaswa ‘kimafia’ ambayo yalitoka kwa Wolper kwenda kwa rafiki yake yakionesha anabanjuka na mwanaume huyo wa mtu aliyejulikana kwa jina moja la Gee.
YADAIWA NI MUME WA SHOSTI YAKE
Chanzo hicho kilikwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba licha ya kuwa ni mume wa mtu, mwanaume huyo ni bwana wa rafiki yake kutokana na mawasiliano hayo yalivyosomeka.
“Mashabiki kila siku huwa wanamtetea Wolper na skendo zake, sasa nakutumia picha pamoja na ‘chating’ zake alizokuwa akichati na shoga yake kuhusiana na jamaa huyo,” kilisema chanzo hicho.
PICHA ZATUA RISASI JUMAMOSI
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wa Risasi Jumamosi alimtafuta sosi huyo na kufanikiwa kuzitia kibindoni picha hizo kisha kazi ya kuwasaka wahusika ikaanza.
Wa kwanza kutafutwa alikuwa ni Gee ambaye kwa mujibu wa vyazo tofauti, ilidaiwa kuwa kwa sasa hayupo Bongo na hakuacha mawasiliano yoyote tangu alipoondoka.
WOLPER SASA!
Baada ya jitihada za kumsaka mwanaume huyo kugonga mwamba, paparazi wetu alimtwangia simu Wolper ambaye alieleza kila kitu:
Paparazi: Mambo vipi Wolper, nasikia makelele unaweza kusogea sehemu yenye utulivu kuna ishu nataka tuongee?
Wolper: Niko msibani na sasa hivi ndiyo zoezi la kuaga mwili, ngoja niingie kwenye gari nikupigie.
Baada ya dakika 45
Wolper: Haya niambie wangu niko sehemu nzuri.
Paparazi: Ni hivi, kuna habari imetufikia ikiambatanishwa na picha na baadhi ya chating inakuhusu wewe!
Wolper: Habari gani hiyo mbona unanitisha?
Paparazi: Kuna picha zinakuonesha wewe ukiwa katika pozi la kimalavidavi na jamaa anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu. Ukiachana na picha hizo, zimeambatanishwa chating zinazoonesha ulikuwa ukichati na rafiki yako kumueleza kuwa mwanaume uliye naye ni mume wa mtu!
Wolper: Kiukweli kabisa bila ya hata kupepesa macho hizo picha ni zangu na zimepigwa kwa kutumia simu yangu tangu mwaka juzi lakini kuhusiana na hizo chating siyo zangu hata wewe unaweza kuwa shahidi kwani mara nyingi huwa tunachati na unajua vizuri ‘floo’ yangu katika kuandika SMS.
Paparazi: Ok, sawa, lakini turudi katika suala la picha, huyu ndiyo bwana’ko wa sasa?
Wolper: Hapana, huyo ni mshikaji wangu tu na tulipiga picha hizo tukiwa baa tena kipindi kile nahamia tu Mwananyamala (Dar) na sasa hivi hata sijui huyo mshikaji yuko wapi.
Paparazi: Ina maana huna mawasiliano naye kwa muda mrefu, mtu ambaye mlipiga naye picha kimahaba namna hii?
Wolper: Kweli kabisa, sina mawasiliano naye kitambo nikimaliza tu kuongea na wewe nitamtafuta na kumuuliza kulikoni picha hizo kuvuja.
Paparazi: Si ulisema umepiga katika simu yako wewe si ndiyo wa kujiuliza kwa nini picha zimevuja?
Wolper: Nilimzawadia simu kama rafiki yangu na picha zikiwa humohumo sikuzifuta.
Paparazi: Haya Wolper ngoja nikuache mi niendelee na majukumu.
Wolper: Poa wangu baadaye nitakucheki.
WOLPER HUYUHUYU
Hii ni mara ya pili kwa Wolper kutuhumiwa kukwapua bwana wa rafiki yake. Hivi karibuni mshiriki wa Miss Tanzania 2012, Husna Maulid alilalamika kuwa Wolper kamchukulia bwana’ke aliyemtaja kwa jina moja la Rajab, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Si Wolper pekee, ‘trendi’ inaonesha kuwa mastaa wengi wa kike hasa wa filamu wamefanya ishu ya kuporana wanaume kuwa sehemu ya utamaduni katika tasnia hiyo bila kujua wanajiondolea heshima mbele ya jamii.

TICKET ZA POOL PARTY YA JUNE 21 ZAANZA KUUZWA

 
tickets sales point yaah!!!ON from today grab early yours hutakiwi kukosa!!its ol abt pool party 21 junee 2014.walkgard hotel
1.mtoka gas point
2.neyma gas point
3.manyema cafe uswahilini
4.shifa cosmetisc migeyo
5.sauti(nkindo)
6.josia kibira university(jokuko)
7.linas night club

Na kwa wale watakao itaji kununua kwa njia ya simu au kufikishiwa walipo wasiliana nasi kwa simu no +255 754429037. wai ticket yako sasa nafasi ni chache sasa nafasi nichache

JIMMY YEYOO NA BK SUNDAY KUIWAKILISHA BUKOBA KWENYE UZINDUZI WA WIMBO ''TUULINDE MUUNGANO'' DODOMA

Jimmy yeyoo akiwa na BKsunday Maandalizi ya tamasha la uzinduzi wa wimbo wa Tuulinde Muungano kwenye uwanja wa Jamhuri,Dodoma leo.

Saturday, June 7, 2014

Hivi Huyu Halima Kimwana ni Nani Kwa Diamond?

Kuna watu wanashangaza kidogo,siyo kwamba tunawafuata majumbani mwao na kugundua tabia zao,kwamba wanakula sana,wachoyo,wachafu au hawapatani na majirani zao,hapana,wanayoyafanya ama kuzungumza,wanatufanya tuwatambue.Lakini tunaishia kuwajua kwa majina na matukio yao.Ukiniuliza babu Tale ni nani,fasta nitakujibu kuwa ni msaidizi wa shughuli za Diamond,Romie Jones nitakuambia ni ndugu yake Diamond,Wema Sepetu,ni usingizi wa Diamond,kwa maana ya mpenzi,lakini ukiniuliza Halima Kimwana ni nani,naweza kulipuuzia swali lako kwa maana sitambui wala kujua ni nani kwa Diamond.
Siwezi kuacha kujiuliza hivi huyu binti wa mjini  ni nani kwa Diamond?rafiki,dada,shemeji yake,mpambe au nani,Au ndiye kiunganishi chake kwa wale viumbe waliosababisha aitwe sukari ya warembo?yeye ni nani haswa hata afikie hatua ya kumchagulia Diamond mpenzi wa kuwa nae,ni nani hasa hata afikie kumaindi uwepo wa Wema kwenye himaya ya Diamond,kajina kake kamezidi kukaa on ea kwa kipindi kirefu kutokana na uwepo wake karibu na Diamond,ana nguvu sana kwa Diamond,Nilipuuzia kwa muda mrefu sana nikiamini ni mtu wake wa karibu wa kumshikia poda awapo lokesheni ya video zake,au anashikilia simu zake awapo stejini,baadae nikadhani kuwa huenda ni msaidizi wa mambo binafsi ya Diamond.Lakini kufikia hatua ya kumpangia Diamond mwanamke  wa kuwa nae,kidogo hapo nashindwa kuelewa,yeye ni nani kwa Diamond?
Wadau mnaojua uhusiano wa huyu dada hebu mtujuze,ni nani,anafanya shuhuli gani,naamini wote mliosoma gazeti hilo mna kiu ya kujua.
Source:Gazeti la KIU ya jibu toleo no 1275 la tarehe 2-5/6/2014 
Via Sintah Blog

Jeshi la Polisi Linadaiwa Kuvamia Nyumbani kwa Lwakatare na Kuwakamata

Taarifa ya awali...
Katika hali ile ile ya mwendelezo wa kutumikia maelekezo na maslahi ya CCM dhidi ya wapinzani wa kisiasa wa chama hicho, Jeshi la Polisi usiku huu limevamia nyumbani kwa Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA, Wilfred Lwakatare na kumkamata housegirl wake.
Kama hiyo haitoshi, jeshi hilo la polisi limewakamata wafanyakazi wengine wawili (house boys) wa Lwakatare. Hadi muda mfupi uliopita vijana hao wawili, walikuwa wako Kituo cha Polisi Mbezi huku msichana wa kazi wakizunguka naye kwenye gari la patrol bila kumfikisha kituoni.
Jeshi hilo la polisi kupitia kituo hicho cha Mbezi lilikuwa linawatisha kila mtu anayekwenda hapo kituoni kuulizia sababu za vijana hao kukamatwa, lakini hatimaye mmoja wa watu walioko kituoni hapo ametonya kuwa polisi wanasema mmoja wa vijana hao kesi yake iko Arusha!
Kijana anayetaka kubambikiwa kesi huko Arusha ni mwanagenzi kabisa mjini. Hata ukimwambia aende Chalinze au Wami hawezi kupajua. 
Hatimaye mbinu za CCM kupitia jeshi la polisi ya kutaka kukichafua CHADEMA au viongozi wake kwa kutumia kes za kubambikia ugaidi imerejea tena...
Tutawaletea taarifa kamili...
JF