POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, February 28, 2014

AKON ASAIDIA BARA LA AFRIKA KWA KUSAMBAZA UMEME KWA MAKAZI ZAIDI YA MILL.1

Si kuamua tu kuongelea suala la kumiliki mke zaidi ya mmoja, kama vile King Mswati.
Staa wa muziki wa Kimataifa,Akon kutoka pande za Senegal ameamua kuligeukia Bara la Afrika na kutoa msaada unaostahili akishirikiana na makampuni yaliyojitolea katika kampeni hiyo iitwayo Akon Lighting Africa.Kwenye mradi wa mazingira wa kusambaza umeme kwenye makazi ya watu barani Afrika.
Inasemekana kwamba mradi huo ambao umekadiriwa kwamba mpaka itakapofika 2015 makazi zaidi ya million 1 barani Afrika yatakuwa yamepatiwa umeme kupitia mradi huo wa kusambaza umeme wa sola.
Tayari ameshatembelea nchi zaidi ya nne kwa ajili ya mradi huo ikiwemo Senegal, Mali, Guinea na Burkina Faso.

PNC AFUNGUKA BAADA YA KUPIGWA PICHA YA UDHALILISHAJI NA USTADHI JUMA NA MUSOMA

Kufuatia picha na video inayomwonyesha Msanii PNC akiwa amempigia magoti Boss wake wa zamani CEO wa mtanashati Ustaadh Juma na musoma, lawama nyingi zimemwangukia Ustaadh kwa kuziweka picha hizo mtandaoni
Siku ya jana PNC hakuweza kupatikana ila leo 255 ya xxl ya clouds fm imepiga naye stori.

KITALE ANUNUA UGOMVI WA PNC BAADA YA KUDHALILISHWA NA USTAADH JUMA NA MUSOMA

Msanii wa Comedy Kitale ameamua kununua ugomvi wa msanii wa Bongo Fleva,PNC na Ustaadh Juma na Musoma baada ya kumdhalilisha msanii huyo kwa kumrekodi video na kumpiga picha na kuzisambaza mtandaoni.Baada kuziona picha hizo Kitale aliamua kumpigia simu Ustaadh Juma na kuuliza kwanini ameamua kufanya kitendo hicho cha kidhalilishaji ambapo Ustaadhi Juma alimjibu mbovu.
Zaidi msikilize Kitale akitiririka.

WAKALI WA SONG LA CHELEWA,NAVY KENZO KUANGUSHA BONGE LA SHOO,MAISHA CLUB JUMAPILI HII

Navy Kenzo chini ya Nah Reel na Aika Jumapili hii watakua na show pande za Maisha Club.
Pia kutakuwa shindano la kudance ambapo litaendeshwa kuwatafuta watu watatu wanakaoweza kwenda sawa na Bokodo Dance na watu hao watatu watashiriki kwenye video ya Chelewa.

MIKE TEE"WASANII TUKIKAA KIMYA KWA HILO LA USTAZ JUMA TUTAKUJA VULIWA NGUO HADHARANI"


Msanii mwenzangu PNC kadhalilishwa sana na OSTADH JUMA kwenye MEDIA zote, me toka jana natafakari sana kwa mtu mzima kufanya kitendo kama kile, upande wangu nimeumia na nimeona kama mimi nimefanyiwa kitendo kile.
Sasa basi wasanii wenzangu, washabiki wetu , viongozi wa ngazi mbalimbali tunajua mambo haya yapo lakini yana kipimo, tukikaa kimya wako watakaotuvua nguo hadharani kisa sisi wasanii ambao tunadharaurika hatuna elimu hatuna kipato ila tunatumika na wachache kupata wanachotaka,
Je tufanye nini me nimeshindwa cha kufanya we need your support wenye uchungu wa muziki wetu na wasanii wa TANZANIA kwa ujumla

Thursday, February 27, 2014

ALI KIBA AELEZEA SABABU ZA UKIMYA WAKE KWENYE GAME YA MUSIC


Kwa kipindi kirefu mkali wa ‘Single Boy’ Ali Kiba amekuwa kimya bila kutoa kazi yake binafsi huku ukimya wake ukizua maswali mengi kwa mashabiki na wadau wa muziki Tanzania.

Lakini leo (February 25) Ali Kiba amezua maswali mengine kwa mashabiki wake baada ya kuweka kwenye Instagram picha inayomuonesha akiwa na AY na Mwana Fa na kuandika ‘@Aytanzania&007#mj record #wait for it bonge ya wimbo.’

Hata hivyo hakuweka wazi kama ni wimbo wake au ameshirikishwa na maswaiba hao.

Tovuti ya Times Fm imefanya mahojiano na Ali Kiba ambaye ameyajibu maswali hayo yote, maswali ambayo hapo awali yalikuwa na majibu ya kuhisia tu bila kuwa na uhakika.

Ali Kiba ameiambia tovuti hii kuwa aliweka picha hiyo kwenye Instagram lakini hakuweka maelezo ya kutosha kwa makusudi.

“Sababu ya kuweka vile ni katika kutaka tu kuwa-surprise watu kwa sababu sikupenda kuwambia ni ngoma ya nani ila nimewajulisha kuwa nimefanya nao na tumefanya kwa MJ, hiyo yote ni kutaka kuwa-surprise.” Amesema Ali Kiba.

Mwimbaji huyo amedai kuwa hadi sasa wimbo huo haujajulikana ni wa nani kati yake yeye, Mwana Fa na AY, “tumefanya wote…haijajulikana ngoma ni ya nani.”

Ali Kiba ameongeza kuwa mashabiki wampe miezi miwili ijayo na kisha watapata maelezo ya kutosha kutoka kwake na kwamba baada ya muda huo kila kitu kitakuwa sawa.

Mwimbaji huyo wa ‘My Everything’ ameeleza pia sababu za yeye kuwa kimya, pamoja na mpango wake kwa mwaka 2014 ambapo amedai kuwa ataachia albam yake mpya.

“Sababu ya kuwa kimya ni kumpush Abdu Kiba aweze kuwa sawa sawa na vilevile mimi ni mzazi kwa hiyo niko busy na jinsi ya kuwa baba. Yaani vitu vingi vyote nilikuwa nikifanya, wakati muda wote niliokuwa nikifanya hivyo vitu nilikuwa najiandaa na albam yangu nyingine ambayo ni ujio mpya…nakuja na everything.

“Albam ipo kwa sababu itakuwa chini ya usimamizi wa kampuni ambayo inanihost, na ndio maana nikakwambia nipe miezi miwili na watu watajua kila kitu kinachoendelea…itafanyika na usimamizi mzuri tu na process zote zitakuwa ziko okay. Ila siwezi kukwambia ntafanya na distributor gani lakini, wasimamizi wangu watafanya hilo, wasimamizi ambao wamenichukua ndio maana ukaona kimya kingi, ni ku-fight maandalizi na kumaliza ngoma.”

Wednesday, February 26, 2014

Baada ya kuhairishwa Valentine Day,uzinduzi wa USIKU WA KIGODORO kufanyika Jumamosi hii,Dar Live

Ile filamu ya Kigodoro ambayo ilihairishwa uzinduzi wake siku ya Valentine mwezi huu,sasa kufanyika Jumamosi hii pande za Dar Live,Mbagala.Muandaaji wa uzinduzi huo,Zamaradi Mketema amesema kwa kushirikiana na Global Publishers walihairisha uzinduzi huo ili kuufanya uwe na burudani za kutosha na kuwapa mashabiki kitu cha uhakika.Alisema kuwa katika uzinduzi huo wa Usiku wa Kigodoro watakuwepo wasanii mbalimbali kama Msagasumu a.k.a Mkali wa Kigodoro, Rihama Ally,Shamsha Ford,Wema Sepetu,Kajala Masanja na wengineo.
Naye Staa wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu amesema kuwa hajawahi kuhudhuria Kigodoro na ana hamu sana ya kukiona na na kuwaambia mashabiki wajitokeze kwa wingi Jumamosi hii