POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, December 17, 2014

Young Suma na GNako waja na collabo


Msanii wa muziki wa bongo flava nchini Tanzania, Young Suma anatarajia kuachia audio ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Hatujivungi’ aliomshirikisha Mfalme wa viitikio ambaye pia ni rapa kutoka kundi kali la muziki lenye makazi yake jijini Arusha, G-Nako hivi karibuni.

Young Suma ameiambia hivisasa blog kuwa wimbo huo utakuwa ni zawadi maalumu kwa mashabiki na wapenzi wa muziki wake hasa katika msimu huu wa sikukuu.

Wimbo ‘Hatujivungi’ umetayarishwa na mtayarishaji mahili nchini, Levybeat ambapo, Young Suma amesema kazi hiyo ni ya kipekee kutokana na style ya kurap na kuimba iliyoitumika pamoja na beat ilivyo kali.

Roboti zapata ajira mgahawani China

 
 Hadimu hivi karibuni huenda wakakosa ajira maana roboti zimezinduka

Mgahawa mmoja nchini China umeanza kutumia Roboti badala ya kuwaajiri hadimu au wafanyakazi wa hotelini kuwapakulia chakula na vinywaji wageni. Hebu tazama mambo yalivyo.CHANZO BBC

Tahadhari:'Hatari za urembo bandia'

              
Huwezi kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo bandia.
Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hii
Kwenye treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna ''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.
Rafiki yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.
'Uasi mkubwa'
Kilio cha uchungu baada ya upasuaji wa pua ili kunyooshwa
Katika nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi ya 'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.
''Msisitizo unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema ''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
'Gharama si mchezo'
Baada ya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti, mawnamke huyu alipata na titi moja kubwa na lengine ndogo
Kim Bok-soon alitumia Won milioni 30 (£17,320) kwa jumla ya upasuaji mara 15 kwenye uso wake katika kipindi cha siku moja na baadaye akagundua kuwa daktari wake hakuwa mpasuaji wa kuongeza urembo bandia mwilini ambaye alimhadaa Kim BoK-Soon kutumia won (17,320) kufanya upasuaji mara 15 kwenye uso wake.
Sehemu ya shida ni kuwa upasuaji wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa hivyo unawaalika madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale waliohitimu katika nyanya zingine za utabibu.
Inadaiwa kuwa taratibu zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi moja kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati mgonjwa wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na kuwacha kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.
Juu ya hiyo, iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza urembo bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.
Kwa uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.
'Biashara kubwa'
Sio China peke yake ambko biashara ya urembo bandia imenoga hata Venezuela ambako wanawake wanapenda sana makalio bandia
Lakini wao wanapigana na mseto huu, Upasuaji una faida sana, hata una bei ambazo zinadhoofisha upasuaji huo Marekani na Ulaya. Ni biashara kubwa sana huko Gangnam, hapa katika Seoul, bei ya "kurekebisha jicho" ni dola 1500 na ni shughuli inayochukua dakka 30 tu. hiyo huongezeka hadi dola 11,000 kwa upasuaji wa kurekebisha sura.
Lakini labda watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa Korea Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia kisu cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye mahakama.
Malkia aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa upasuaji wa kukuza kifua ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani upasuaji huo ulifanya titi lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.
Analaumu madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ". Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama madawa ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."
Na madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji" Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni juu yako mwenyewe.

Ebola:Msako wa wagonjwa kufanywa S.Leone

 
Rais wa Sierra Leone Ernest Bai Koroma ametaka kufanyika kwa msako wa nyumba hadi nyumba kwa waathiriwa wa ugonjwa wa ebola nchini humo.
Rais Ernest Bai Koroma wa Sierra Leone amesema kuwa msako wa nyumba kwa nyumba unaanza kote nchini humo kuwatambua watu walio na ugonjwa hatari wa ebola.
Aidha, Rais huyo amepiga marufuku biashara siku ya Jumapili.
Katika hotuba kupitia televisheni ya taifa, Koroma amesema kwamba usafiri kutoka wilaya moja hadi nyingine ni marufuku.
Juma moja lililopita, wakuu walifutilia mbali mikutano yote na sherehe za siku kuu ya krismasi na mwaka mpya kama njia ya kukabiliana na kusambaa zaidi kwa ebola.
Kwa mujibu wa takwimu za hivi punde kutoka shirika la afya Duniani WHO, Sierra Leone ni taifa ambalo limeathirika pakubwa na ebola ambapo zaidi ya visa elfu nane vimeripotiwa.
Maafisa wa kukabiliana na Ebola wakitembea katika mitaa ya Sierra Leone.
''Musiwafiche wagonjwa'',alisema rais.
Mbali na kufutilia mbali biashara za siku ya jumapili,mikakati hiyo mipya itashirikisha mda wa kununua bidhaa siku ya jumamosi na katikati ya wiki.
Mji wa Freetown umerekodi zaidi ya asilimia 50 ya maambukizi ya ugonjwa wa ebola nchini Sierra leone katika kipindi cha majuma mawili yaliopita.
Mwandishi wa BBC nchini Sierra Leone Umaru Fafana amesema kuwa mikakati hiyo inalenga kudhibiti makundi ya watu.
Amesema kuwa wakaazi wa mji wa Freetown wanaendelea kujumuika katika barabara mbali na kufanya mazoezi kwa pamoja licha ya tishio hilo la Ebola.

MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA MWANAMUZIKI SHEM KARENGA

Sehemu ya jeneza la marehemu Karenga.…

Sehemu ya jeneza la marehemu Karenga.
Mwili ukisitiliwa kaburini.
Umati uliojitokeza katika mazishi.
Mtoto wa Karenga aitwaye Karenga (kushoto) akiwa na mmoja wa wanandugu.
Baadhi ya wanamuziki waliohudhuria mazishi hayo.
HATIMAYE mwili wa aliyekuwa mwanamuziki mkongwe nchini na nje ya nchi, Shem Karenga,  umezikwa jana katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar e Salaam.
Karenga aliwahi kutamba na nyimbo nyingi ukiwemo ya Dada Asha,  ambao ulivuma sana Afrika Mashariki na Kati.Mazishi hayo yalihudhuriwa na mamia ya watu wakiwemo wanamuziki.Kujua mengi tembelea www.globaltvtz.com

MIKATABA YA KIMATAIFA YAISAIDIA TANZANIA HIFADHI YA JAMII

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima. Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha…

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana (kulia) akizungumza katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii unaotarajiwa kumalizika leo jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Kebwe Stephen Kebwe na kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.Mkurugenzi mshiriki anayeshughulikia masuala ya program kutoka makao makuu ya UNICEF, Bi. Alexander Yuster, akiibua hoja kwenye mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii ulioandaliwa na serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha na wadau wengine kwa lengo la kubadilishana uzoefu juu ya nini cha kufanya kusaidia makundi maalumu katika jamii unaomalizika leo jijini Arusha. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom.Baadhi ya washiriki wa mkutano mkubwa wa kimataifa wa hifadhi ya jamii wakiwemo watengeneza sera, watafiti na waendeshaji wa mifuko ya hifadhi kutoka mataifa ya Kenya, Uganda, Bangladesh, Mozambique, Lesotho, Malawi, Afrika Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Sudan Kusini na wenyeji Tanzania unaoendelea jijini Arusha.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
UTIAJI saini wa mikataba ya kimataifa, inayohusu hifadhi ya jamii kumeiwezesha Tanzania kuwa katika hatua nzuri ya kutekeleza ajenda yake ya kuhakikisha kwamba wananchi wake wanakuwa na haki sawa katika kujipatia maendeleo na ustawi.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk Pindi Chana katika mkutano wa siku tatu wa kimataifa unaohusu hifadhi ya jamii mjini hapa.
Alisema mikataba mikubwa ya kimataifa ambayo Bunge la Tanzania limeridhia na iliyoleta mabadiliko makubwa katika sera na sheria nchini ni pamoja na Mkataba wa Kufuta Aina zote za Ubaguzi na Unyanyasaji kwa Wanawake (CEDAW) wa mwaka 1979, Mkataba wa Haki za Watoto (CRC) wa mwaka 1989 na Mkataba wa Afrika wa Haki za Watoto.
Mikataba mingine ni Mpango wa Maendeleo wa Milenia (MDGs), Azimio la Umoja wa Mataifa Namba 1325 la mwaka 2000 na Azimio Namba 1820 la 2006, ambayo inazungumzia ushiriki na uwezeshaji wa wanawake katika kutanzua migogoro na ujenzi wa taifa.
Alisema kitendo cha kuridhia kwa mikataba na maazimio hayo, kinaonesha ni kwa namna gani serikali ina utashi wa utekelezaji wa maazimio hayo kwa lengo la kuhakikisha watoto na wanawake, wanalindwa dhidi ya vurugu za aina zozote na kuwanyima haki zao za msingi.
Dk.Chana alisema kwa kuzingatia ushiriki kuleta katika maendeleo ya nchi, Tanzania imetayarishwa Dira ya Maendeleo ya 2025 ikiwa na vipengele vyote vya haki vyenye lengo la kuongeza wigo wa ushiriki wa wanawake.
Aidha, ili kuhakikisha makundi maalumu yanalindwa, serikali pia imetengeneza Sera ya Maendeleo ya Watoto ya mwaka 2008, ambayo kwa sasa inapitiwa ili kuingiza mambo mengine yanayohusu haki za mtoto.
Aidha, ikiwa imejikita kuondoa masuala ya kuondoa udhalilishaji wa kijinsia, serikali imefanya maamuzi mengi yenye manufaa pamoja na kushirikiana na wadau binafsi kuboresha maisha ya watanzania.
Alisema kwamba suala la wanawake na maendeleo, limeingizwa katika mkakati wa taifa wa kupunguza umaskini. Alisema mwaka jana serikali ilitengeneza programu ya taifa inayohusu wadau wengi ya miaka mitatu ya kuondokana na ukatili kwa watoto.
Mkutano huo unaozungumzia hifadhi, ulifunguliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi ambaye alisema misingi imara imeshawekwa kusaidia hifadhi ya jamii kuelekea dira ya taifa ya kuwa na kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA ELIMU YAANZA LEO JIJINI DAR

Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel (Wa pili kutoka kulia) akiwaonyesha ramani ya maonyesho ya Kimataifa ya Elimu kwa wadau wa Elimu waliojitokeza kushiriki maonyesho yanayoanza Leo Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa…
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel (Wa pili kutoka kulia) akiwaonyesha ramani ya maonyesho ya Kimataifa ya Elimu kwa wadau wa Elimu waliojitokeza kushiriki maonyesho yanayoanza Leo Desemba 17-21, 2014 katika viwanja Mwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akielezea maonyesho ya Kimataifa ya Elimu yanayoanza kesho Desemba 17-21, 2014 katika viwanja vyaMwalimu Julius Kambarage Nyerere vilivyoko Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Uwakala wa Vyuo kutoka Nje Global Education Link Bw. Abdulmalik Mollel akiwakaribisha wagei katika ofisi za GEL.