POOL PARTY
Friday, March 14, 2014
RAY C:RAFIKI WA KWELI UTAMJUA KWENYE MATATIZO
MSANII IBRA DA HUSTLER APELEKWA REHAB NA MAMA YAKE BAADA YA KUZIDIWA NA MADAWA YA KULEVYA
BARNABA KUANZISHWA KIPINDI KIPYA CHA TV,KUWA HEWANI JUNI MWAKA HUU
Thursday, March 13, 2014
Hata kama akifa kesho: Huyu ndio msanii Diamond anamuaminia kuipeperusha bendera ya Tanzania kimuziki
Watu wote tunajua kuwa Diamond ni mmoja wa wasanii wanaoipeperusha
bendera ya Tanzania ki-muziki katika nchi mbali mbalii nje na ndani ya
Africa, kwa kufanya Collable na wasanii wa nje ya Tanzania, kwa
kutengeneza video zenye quality ya juu na kusababisha kuchezwa katika Tv
za Nje ya Africa nk. lakini huyu ndio msanii ambae yeye anamuaminia ,
na hata kudiriki kumuandika katika acc yake ya Instagram kuwa ndio
msanii atakaeipeperusha bendera ta Tanzania hata kama yeye atakufa kesho
WEMA, AUNT WALA KICHAPO
KIMEWAKA! Habari zilizothibitishwa zinaeleza kuwa, sura mbili za mauzo kwenye sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu na Aunt Ezekiel Grayson wanadaiwa kula kichapo kutoka kwa msanii mwenzao, Adam Kuambiana, Amani limeinyaka.
Tukio hilo lililoshuhudiwa na ‘shushushu’ wetu lilijiri mchana kweupe maeneo ya Mikocheni, Dar, hivi karibuni baada ya kuibuka timbwili lenye ujazo wa kilo kadhaa baina ya mastaa hao.
ALIANZA WEMA
Kwa mujibu wa chanzo, Wema ndiye aliyeanza kummwagia Kuambiana maneno ya shombo akimwambia kuwa ahakikishe siku hiyo haipiti bila kukata kucha za miguuni kwani ni ndefu na zinatisha.
“Mwanzoni ilikuwa kama utani tu. Wema alimwambia Kuambiana akate kucha, tena itabidi atumie mkasi wa kukatia michongoma maana kwa wembe hazikatiki.
“Pia Wema alimwambia yeye hawezi kumwacha mpenzi wake na kucha ndefu kama hizo za Kuambiana,” kilisema chanzo chetu.
Ilizidi kudaiwa kwamba wakati Wema akiendelea ‘kumpaka’ Kuambiana, Aunt aliyekuwa amejilaza chini alidakia na kusikika akisema kuwa ni kweli msanii huyo mwenye uwezo wa juu katika fani anatakiwa kukata kucha hizo huku akizungumza maneno ya shombo kwa jamaa huyo.
HASIRA
“Baada ya kuona imekuwa ‘too much’, Kuambiana alipandwa na hasira, akanyanyuka kwenye kochi na kumfuata Wema kwa lengo la kumpa kipigo,” kilisema chanzo hicho.
MARTIN KADINDA AMUOKOA
Habari zilidai kwamba, Kuambiana alipomfikia Wema alianza kumpiga vibao hadi meneja wake, Martin Kadinda akaingilia kati kumuokoa mwanadada huyo ambaye pia ni meneja wake.
KIBAO CHAMGEUKIA AUNT
Chanzo kilieleza kwamba baada ya kuachana na Wema, msaanii huyo ambaye pia ni ‘dairekta’ wa sinema mbalimbali za Bongo alimfuata Aunt na kuanza kumlamba makofi ya kutosha.
Tukio hilo lilizua tafrani na kuwafanya wasanii wengine waliokuwa eneo hilo wakimbie na kushindwa kuwatetea Aunt na Wema kwa kuogopa kugeuziwa kibao.
KUAMBIANA ANASEMAJE?
Baada ya kuinyaka ishu hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta Kuambiana na kumuuliza kulikoni kugeuka bondia na kuwapiga warembo hao ambapo alikiri kutokea kwa ishu huyo.
Alisema kuwa, Wema na Aunt ni kama wadogo zake, tena yeye kama dairekta wao walipaswa kumheshimu na siyo kumvunjia heshima.
“Akina Wema ni wadogo zangu, wanahitaji kuniheshimu na mimi ndiye mwongozaji wa filamu yao, kwa nini wanikosee heshima? Hata kama wamekasirika lakini nimewashikisha adabu,” alisema Kuambiana kwa ile sauti yake nzito.
WEMA & AUNT
Kwa upande wao, walipoulizwa Aunt na Wema kuhusiana na kichapo walichopewa walisema walishamzoea jamaa huyo, lakini kwa alilolifanya la kuwapiga makofi aliwakwaza kwa sababu hata kama ni mwongozaji wa filamu yao lakini alikuwa pale kwa ajili yao.
HISTORIA YA KUAMBIANA
Ukiachana na tuki hilo, Kuambiana anadaiwa kuwa na mkono mwepesi hasa anapokuwa ‘lokesheni’ ambapo mwaka jana, aliwahi kumtia mikononi staa mwingine wa filamu za Bongo, Rose Ndauka walipokuwa wakirekodi filamu visiwani Zanzibar.
Siku ya tukio hilo, Kuambiana alikuwa akidairekti Filamu ya Distress in Zanzibar. Alimshutumu Rose kuvaa mavazi tofauti na maagizo yake, katika kujibishana akamuwasha makofi.
HATA MITAANI!
Juni, mwaka jana, Kuambiana alimshushia kipigo Fadhili Joseph ambaye alimdai fedha za bia alizokunywa kwenye baa yake, Sinza, Dar es Salaam.
Kuambiana aliposhindwa kulipa aliacha laptop (kompyuta mpakato), siku iliyofuata alirudi na kushusha kichapo huku akiitaka laptop hiyo.
Kuambiana alikamatwa na Polisi Kawe, Dar kwa faili la malalamiko KW/RB/5761/2012 SHAMBULIO. Kesi hiyo ikahamishiwa Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Mabatini’ kwa vile ndiyo kituo cha karibu na eneo la tukio.
MADAIREKTA WAKOJE?
Mbali na Kuambiana, staa mwingine ambaye pia ni dairekta wa muvi za Bongo, Issa Musa ‘Cloud’ naye aliwahi kutoa kipigo cha bakora kwa msanii Blandina Chagula ‘Johari’ kwa kosa la kuchelewa kufika sehemu ya kurekodia filamu.
ALI KIBA KUTISHIWA KUUAWA, DIAMOND KUHOJIWA POLISI
Andrew Carlos na Shakoor Jongo
SAKATA la staa wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ kunusurika kuuawa na watu wasiojulikana kwa kutumia bastola limechukua sura mpya, safari hii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa amejiandaa kuhojiwa na polisi.
SAKATA la staa wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ kunusurika kuuawa na watu wasiojulikana kwa kutumia bastola limechukua sura mpya, safari hii, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amefunguka kuwa amejiandaa kuhojiwa na polisi.
Kwa mujibu wa chanzo chetu katika jeshi hilo jijini Dar, Diamond ambaye
amekuwa akitajwa sana katika sakata hilo kupitia mitandao ya kijamii
ataitwa kuhojiwa.
“Unajua ile kesi ipo hapa Central, awali ilitokea Polisi Msimbazi, sasa
mpelelezi wake amekuwa akifikiria kumwita Diamond ili amhoji maana
anatajwa sana,” kilisema chanzo hicho.
Hivi karibuni, Ali Kiba alivamiwa usiku na watu zaidi ya watano nyumbani
kwao, Kariakoo jijini Dar ambapo waliruka ukuta na kuingia ndani huku
kila mmoja akiwa na bastola.
Ilidaiwa kuwa, mmoja kati ya watu hao ambao ilisemekana walitumwa kumuua
msanii huyo, aliibua mzozo wa makusudi kwa wenzake ili kumpa mwanya
Kiba kutoroka kwa vile hakufurahishwa na kitendo hicho.
Habari zinasema walipoingia ndani huku kelele za mbwa zikasaidia
kumshtua staa huyo, ule mzozo ulioanzishwa na wavamizi hao ulimsaidia
Kiba kutoroka ingawa walimkosakosa risasi.
Ikasemekana baada ya msanii huyo kukimbia, jamaa ambaye alimkingia kifua
alimpigia simu na kumfungukia watu waliohusika huku ikidaiwa kuwa
baadhi yao ni mastaa wenzake.
“Alinitajia tu majina lakini nilishindwa kuthibitisha moja kwa moja
hivyo nikayafikisha Kituo Kikuu cha Polisi (Central) kwa ajili ya
uchunguzi,” alisema Ali Kiba huku akikataa kutaja hata jina moja.
Hata hivyo, mengine yaliibuka hasa kwenye mitandao ya kijamii kuwa,
miongoni mwa wasanii waliohusika katika tukio hilo eti ni na Diamond.
Amani lilimsaka afande mmoja ambaye anajua mwenendo wa kesi hiyo ambaye
alikiri kesi hiyo kuwepo Central lakini alisema mambo yote ni siri ya
kazi.
“Nani atahojiwa, nani hatahojiwa ni siri ya kazi yetu,” alisema.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.
Juzi, paparazi wetu walimtafuta staa huyo wa Wimbo wa Number One ili kusikia anazungumziaje manenomaneno hayo ya kwenye mitandao na vinywa vya watu.
“Nimeshasikia nikitajwa katika hilo, kimsingi ni madai mazito lakini
mimi nipo tayari kuhojiwa ili sheria ichukue mkondo wake kwani najua si
kweli na sijui lolote,” alisema Diamond.
Akandelea: “Mimi na Kiba kuna ugomvi gani hadi nifikie hatua hiyo. Kwanza sina moyo wala uwezo wa kufanya hivyo.”
NGUVU YA POMBE YAMUADHILISHA MISS HUYU "REHEMA FABIAN"
Subscribe to:
Posts (Atom)




