POOL PARTY
Saturday, September 14, 2013
JE! ILIKUWA SAHIHI KWA DIAMOND KUMNUNULIA GARI YA KWANZA MZEE GURUMO?
Mara ya kwanza niliposikia Mzee Gurumo wa Msondo Ngoma anadai ameimba zaidi ya miaka 50 na maisha yake bado ya kawaida sana na hakuwahi hata kumiliki gari toka enzi hizo' niliona kuna kitu hakiko sawa... sikuwa na ushahidi tu lakini nilikuwa na uhakika kwa vyovyote vile 'atakuwa alichezea maisha ujanani'
Siku si nyingi tulioona akifanyiwa interview na Salama kipindi cha MKASI watakubaliana na mimi huyu Mzee na wengine wengi tunaosikia
wakihojiwa na vyombo vya habari ..wakilaumu serikali kwa kutowajali. Wengi wao walipata 'golden opportunities' za kuwa na maisha bora lakini 'walichezea pesa' na 'opportunities hizo' so many times...
Mfano: Mzee Gurumo alisema alilipwa 'elfu ishirini' mwaka 1978 ili kuhamia bendi ya Sikinde...kumbuka kuwa Mshahara wa Rias mwinyi mwaka 1992 ulikuwa 'elfu ishirini na saba tu' sasa pata picha huyu mzee alikuwa na pesa kiasi gani? Na mshahara wake ulikuwa 'shilingi elfu tatu' mwaka huo 1978... wakati kima cha chini mpaka mwaka 1987 kilikuwa hakijafika 'shilingi elfu saba'
Kuna Mzee mwingine alitunga kitabu riwaya 'Simu ya Kifo' alilipwa 'elfu kumi na mbili ' miaka hiyo nyumba Kariakoo zinauzwa shilingi 'mia nne' na alikufa bila nyumba wala kibanda..
Orodha ni ndefu...na wapo wengine Baba zetu, Wajomba, babu na kadhalika ukiwaona uzeeni wanavyolalamika na kuomba wasaidiwe.... utasema hawakupata chochote ujanani kumbe anasa, starehe na kuhonga wanawake ndo sababu....
Ukweli ni kwamba watu 'huchezea maisha mno' halafu uzeeni hutafuta wa kumpa lawama mara watoto, mara serikali na kadhalika....
Huyu Mzee Gurumo alikuwa sio mtu wa kupewa gari na Diamond... angekuwa na magari na majumba tele ya kuwarithisha watoto na wajukuu...Am just Thinking Aloud tu kwasababu nimeanza kusikia umaarufu wa huyu Mzee katika Music Toka Nizaliwe Hajawahi Kuchuja.....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment