POOL PARTY

POOL PARTY

Thursday, June 5, 2014

Mmiliki wa nyimbo za Bob Marley aamuliwa...

Bob Marley
Mzozo wa kisheria juu ya nani anayemiliki baadhi ya nyimbo maarufu za reggae duniani umemalizika mjini London.
Nyimbo hizo zilizotungwa na kuimbwa na msanii Bob Marley zimekuwa ziking'ang'aniwa na kampuni 2 pinzani juu ya umiliki wao.
Jaji katika mahakama kuu, Richard Meade alikata kesi ambapo kampuni ya Cayman Music ilikuwa inadai kumiliki nyimbo 13, miongoni mwao wimbo uliopata umaarufu 'No Woman, No Cry' kuwa haina haki nazo tena.
Kampuni hiyo ilikuwa imedai kuwa nyimbo hizo hazikujumuishwa walipouza baadhi ya haki zake kwa kampuni nyingine mnamo mwaka wa 1992.
Kampuni ya Cayman imesema kuwa Bob Marley aliandika nyimbo hizo chini ya majina tofauti, lakini Jaji ameamua kuwa bado kandarasi waliouzia inafunika nyimbo zote hizo.
Bob Marley alifariki mwaka wa 1981 baada ya kuugua maradhi ya saratani kwa muda.

WEMA,AUNTY NA SHILOLE WALIPULIWA BUNGENI KUWA NI VINARA WA KUVAA NGUO ZISIZO ZA MAADILI

 
Ukiukwaji wa maadili ni sehemu ya kilio cha jamii ya watanzania na tayari kilio hicho kimeifikia serikali ambayo imechukua hatua za awali ya kuwaonya watu wanaofanya tabia hizo.Naibu Waziri wa habari,Vijana, Utamaduni na Michezo Juma Nkamia ameeleza hatua ambazo wizara hiyo imechukua katika kukomesha ukiukwaji wa maadili unaofanywa hasa katika kumbi za starehe.Akijibu swali lililoulizwa na mbunge Catherine Magige, Nkamia amesema kuwa serikali imefanya vikao na wamiliki wa kumbi za starehe, wamiliki wa bendi, maafisa wa utamaduni, na wakuu wa polisi.
Amesema serikali imezuia kutoa vibali kwa vikundi vya ‘Kangamoko’ kutokana na uchezaji wake kutofuata maadili na kutoa mfano wa wasanii ambao wamepewa onyo.
“Mfano wasanii waliopewa onyo ni Nay wa Mitego, Shilole na Anti Ezekiel. Na kwa upande wa kumbi ni Mamas &Papas.” Amesema

Naibu waziri huyo ameeleza kuwa serikali imeunda kamati ya kitaifa yakuzuia ukatili, unyanyasaji wa watu wenye ulemavu wa ngozi na watoto na pia udhalilishaji wa wanawake.

UKIKUTANA NA MHESHIMIWA RAIS WA NCHI UTAMUELEZA SHIDA GANI?

Kwa upande wa Staa wa Bongo Fleva,Diamond Platnumz hivi karibuni alipoenda nchini Marekani alipata nafasi ya kukutana na rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania,Dr Jakaya Mrisho Kikwete na alipoulizwa akamwambia shida yake ni kufanya kolabo na wasanii wakubwa, ambapo rais Kikwete alimkutanisha Diamond na mdau mkubwa wa muziki aliyewahi kuwa rais wa record label kubwa ya Def Jam, na makamu wa rais wa Island Def Jam.Mchana huu Diamond anatarajia kupaa kuelekea South Africa kwa ajili ya tuzo za MTV zinazotarajiwa kufanyika Jumamosi wiki hii, na alikua na haya ya kusema kwa mashabiki wake.

Aunt Lulu Alia Kukosa Bwana wa Kizungu kutoka Thailand

Na Hamida Hassan

MKALI wa sinema za Kibongo, Lulu Semagongo ‘Aunt Lulu’ amefunguka kuwa anasikitika kukosa bwana aliyeahidiwa na marehemu Amina Ngaluma.

Akizungumza na paparazi wetu, Aunt Lulu alisema kabla marehemu Amina hajapatwa na mauti nchini Thailand, alimuahidi kumtafutia bwana nchini humo lakini mauti yalimkuta kabla hajamtimizia ahadi hiyo.

“We acha tu, aliniahidi kunitafutia mume baada ya kugundua nasumbuliwa na wanaume kila wakati lakini ndiyo hivyo tena Mungu akamchukua kabla hajanitimizia ahadi,” alisema Aunt Lulu.
Amina alifariki mwezi uliopita nchini humo ambapo chanzo cha kifo chake kikielezwa kuwa ni uvimbe kwenye kichwa.

Huyu ndiye binti anayedai kubakwa na mume wa Flora Mbasha

Huyu Ndio Msichana Ambaye Anahusika na Sakata linaloongelewa sana la Mume wa Flora Mbasha Kumbaka Shemeji yake...Basi huyu Ndio Shemeji Mwenyewe Wajameni
Angalia muonekano wake utapata maswali mengi.

Thursday, April 24, 2014

Wema awapoteza Lulu,Jokate,Wolper,Nelly kwenye shindano la Ijumaa Sexiest Girl 2013-2014


STAA wa filamu za Kibongo,Wema Sepetu ameibuka kidedea kwenye shindano la Ijumaa Sexiest Girl kwa kura 370 huku mshindi wa pili Elizabeth Michael'Lulu' akipata kura 340 akifuatiwa na Nelly Kamwelu.

Shindano hilo lilifanyika katika viwanja Dar Live ,Mbagala usiku wa kuamkia leo  na limeandaliwa na Global Publishers huku burudani ikisindizwa kutoka kwa Weusi(Nikki wa Pili,Joh Makini,G Nako) na Mkubwa na Wanae.










SHILOLE"NILIPEWA MIMBA NIKIWA NA MIAKA 14


Ni msanii mwenye ups and downs nyingi sana , kama unatafuta role model hapa bongo basi muite Shilole. Alianzia kwenye movie lakini kabla ya movie alishawahi kuuza chakula na biashara mbali mbali in order to survive.

Shilole katika pitapita zake kwa bahati mbaya alijikuta akilazishwa mapenzi wakati akiwa na umri mdogo sana, msanii huyo akiwa na miaka 14 tu alijikuta akiwa na mimba . “nilipata mimba nikiwa mdogo sana yani hata maziwa ndio yanaanza sipendi kitu hiki kimtokee msichana mwengine kwa kweli na pia kwa wale wanaume wenye tamaa plz wanapoteza future za watu” alisema  shilole.

Baada yakupata mtoto wake huyo, aliangaika nae na baadae alijikuta akiolewa na mtu mwingine na kuweza kupata mtoto wake wa pili akiwa na umri wa 18 na mwisho wa siku alitoka ndani ya ndoa na kuhamia Dar na kuanza maisha upya.