POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, March 5, 2014

NANII ANAFAA KUCHUKUA TUZO YA BUKOBA MOVIE STAR??

 ONYANGO 20

JAY WA RAZA NO.4

 KIJEBA NO. 1
 ORDER MAN 21
 
HASSAN NO. 5

 . JACK NO.18
JUNIOR NO. 3
 
TESSO BOY NO.2
 FASIA 10


Ili kumpata star wa kuchukua tuzo ya movie star bukoba unaweza kufika viwanja vya kiloyera beach au pia unaweza kupiga kula hizo kupitia kipindi cha THE BASH  kupitia vision fm radio.
       MATUKIO JUMA LA PILI KATIKA VIWANJA VYA KILOYERA BEACH
TESO AKIWA NA FASIA WAKIPIGA KAMPENI KULA MAJI YA MOTO
 MC AMANI KABUGA AKIWA NAMDAU DJ SLAY
 wakati wa uchaguzi.



 ORDER MAN MSHILIKI MWENYE USAJILI WA NAMBA 21 AONGOZA KWA KULA 360.

NIKIWA NA DJ SLAY SISI SOTE NI WATU WA MEDIA


Sunday, March 2, 2014

CHRISS BROWN AZIDI KUPATA MAJANGA..MAHAKAMA YAAMURU ARUDISHWE REHAB

Baada ya kukaa rehab kwa ajili ya anger management na msimamizi wa rehab hiyo kusema kwamba Chris Brown ameonyesha improvement, bado jaji wa kesi hiyo hakuridhika na ripoti na kumrudisha Chris Brown rehab kwa miezi miwili zaidi.
Chris Brown mwenye miaka 24 baada ya maamuzi hayo ya mahakama ali-tweet “Never really goes the way u plan. #LIFE”.

Chris Brown anategemea kutoa The X album tarehe 5 mwezi 5 lakini wasiwasi unakuja kama muda huo wa miezi miwili utaathiri utoaji wa album hiyo ambayo ilitakiwa kutoka tangu mwaka jana.

LUPITA NYONG'O "NILIVYO KUWA MDOGO NILIKUWA NIKIOMBA MUNGU NIPATE NGOZI NYEUPE"


Muigizaji wa Kenya Lupita Nyong’o amesema kuwa alipokuwa mdogo alikuwa akimuomba Mungu kila mara amsaidie awe na ngozi nyeupe sababu alikuwa akiamini kuwa na ngozi nyeusi ni laana.

Lupita ameyasema hayo alhamisi hii alipohudhuria katika ‘Essence Black Women in Hollywood Luncheon’.

Aliongeza kuwa alikuwa anajionea aibu kiasi cha kushindwa hata kujitazama kwenye kioo, mpaka alipokuja kuanza kupata ujasiri baada ya kumuona super model Alek Wek mwenye ngozi nyeusi akisifiwa na watu kama Oprah kama mwanamke mrembo.

Nyong’o aliongeza kuwa hapo ndipo alipoanza kujifunza kuwa uzuri unakuja kwa mtu yeyote bila kujali rangi ya ngozi yake, hivyo anaamini hiyo pia itawahamasisha wasichana wengine ambao wamekutana na hali kama hiyo.

Lupita alielezea hadithi yake ya utotoni baada ya kupokea barua kutoka kwa binti mdogo aliyemwelezea kuwa anaona Lupita kama mwenye bahati kwa kuwa na mafanikio aliyonayo Hollywood huku akiwa ni ngozi nyeusi. Binti huyo aliendelea kusema kuwa alikuwa anakaribia kuanza mchakato wa kubadili rangi ya ngozi yake mpaka alipoanza kumuona Lupita ambaye ana rangi kama ya kwake na bado amefanikiwa.

“I’m honored to be a symbol of hope to others like the women I used to watch made me feel. I hope my presence on screen leads other little girls on a similar journey [to] feel the validation of your own beauty inside and out.” Alisema Lupita.

SIX PACKS ZA DIAMOND ZAWAPAGAWISHA MABINTI WA KI KENYA