POOL PARTY

POOL PARTY

Friday, February 28, 2014

WEMA SEPETU AKIRI KUNENEPA SABABU YUPO KIMAPENZI NA MTU AMPENDAYE KULIKO WOTE


Jana katika Kipindi cha leo Tena Mwanadada Wema Sepetu Aliulizwa kwanini Siku hizi ananenepa sana kiumbo na Mwanadada huyo mrembo alijibu moja kwa moja kuwa ananenepa kwa sababu ana amani ya moyo kwa vile yupo na mtu kimapenzi ampendaye kuliko wote duniani...Nadhani wote mnamjua ni nani?  Mapenzi raha Bwana asikwambie mtu ukimpata akupendaye na wewe anakupenda lazima unenepe

KAMA ULIKUWA HUJUI BASI HEMEDY PHD NA NAJMA SASA NG'ARE NG'ARE



Nimekutana na hizi picha za Hemedy akimbusu msanii wa muziki na filamu Najma na maneno yalioambatana na picha hizo yakizungumzia ndoa na harusi....Huenda sasa hawa ni mambo safi ...Najma alikuwa ni mpenzi wa Mr Blue zamani ......

SAKATA LA MGAGA WA DIAMOND: MKE WA MWENYE GARI LILILOIBWA AIBUKA, AFUNGUKA

Stori:  Sifael Paul
Lile sakata la kukamatwa kwa yule mganga wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya kwa msala wa wizi wa gari, limechukua sura mpya baada ya mke wa mwenye gari, Edric Magayane kuibuka na kufunguka mazito.
Mganga wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Ustadh Yahya.
Akizungumza na gazeti hili, mke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Emida Denson alisema kuwa gari hilo aina ya Toyota Rav4 lilikuwa mali ya familia kabla ya mumewe kudai lilipata ajali hivyo lipo gereji.
Alisema kuwa baadaye mumewe alidai kuwa aliliuza akaongezea fedha kisha akanunua lingine aina ya Toyota Prado.
Alisema habari kuwa gari hilo liliibwa maeneo ya Kariakoo-Msimbazi, Dar hazikuwa za kweli kwani ukweli ni kwamba mumewe huyo alikuwa amemhonga mwanamke aliyemtaja kwa jina moja la Mwanahamis.
“Huyo Mwanahamis amenisababishia mateso makubwa kwenye ndoa yangu karibia miaka miwili sasa. Yaani ndoa yangu ni sarakasi tupu kwa sababu yake.
Edric Magayane na mkewe Emida Denson.
“Ukweli ni kwamba baada ya kuhongwa lile gari alikuwa hajui kuliendesha. Alichokifanya akamwachia Ustadh. Hayo mengine ya kushirikiana juu ya biashara zao za uganga hayanihusu.
“Sasa basi baada ya kuona gari liko mikononi mwa Ustadh ndipo mume wangu akalitaka ndiyo maana wamefikia hapo.
“Kinachoniuma ni kwamba mbali na gari, mume wangu alifikia hatua ya kuja kumpangishia Mwanahamis jirani na nyumba yetu maeneo ya Machimbo-Mwisho wa Lami (Yombo jijini Dar)
“Mbaya zaidi watu wakawa wanamuona mume wangu akiingia kwa Mwanahamis, nimedhalilika sana.
“Nalea watoto wanne peke yangu, wakwangu wawili na wawili wa mume wangu kwa mwanamke mwingine.
Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
“Baada ya kuona ndoa inanitesa nilikwenda kwa mchungaji Kimaro aliyefungisha ndoa yetu kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kariakoo nikamweleza mateso ninayopata.
“Alituita wote, akasemwa lakini baada ya hapo manyanyaso yakaendelea japo walihamia Banana-Ukonga ndiko wanakoishi hadi leo.
“Pia nilikwenda kwenye Dawati la Jinsia wilayani Temeke na baadaye Ustawi wa Jamii.
“Huko kote ilishindikana na sasa bora anipe talaka yangu tugawane mali kwa sababu nilipokutana naye hakuwa na kitu chochote, tulikuwa tukilala chini,” alisema mwanamke huyo kwa uchungu huku akitoa cheti cha ndoa (nakala ipo).
Kwa upande wake mume wa mwanamke alipotafutwa na kusomewa mlolongo wa sarakasi alizozieleza mkewe, alisema kuwa gari hilo lilikuwa mali yake na kwamba lilipata ajali likakaa gereji muda mrefu na lilipopona alikuwa akilitumia mwenyewe.
Kuhusu kuwa na hawara Mwanahamis, jamaa huyo alidai kwamba aliamua kuwa na mwanamke huyo kwa kuwa mkewe alikuwa ana matatizo ambayo hata hivyo hakutaka kuyaainisha.
“Naishi naye (mkewe) lakini kila mtu na chumba chake, huyo mwanamke ana matatizo yake ndiyo maana nikatafuta mtu mwingine, hizo habari anazolalamika, anazusha tu, nimempa uhuru aniache na wangu na yeye atafute mwanaume mwingine,” alisema mwanaume huyo.
Kuhusu gari analodaiwa kukutwa nalo mganga wa Diamond, habari zilieleza kuwa Ustadh aliachiwa kwa dhamana na bado gari hilo lipo mikononi mwa polisi likisubiri kesi kwenda mahakamani.

MASKINI AFANDE SELE

Stori:  Erick Evarist na Joseph Shaluwa
SIKU chache baada ya kuzagaa kwa taarifa za kuachana na mkewe mama Tunda, mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘Afande Sele’ ameibuka na kusimulia mambo ya kusikitisha waliyopita katika safari ya maisha yao.
Mfalme wa Rhymes, Seleman Msindi ‘Afande Sele’.
Akizungumza na wanahabari wetu ndani ya Ukumbi wa Meeda, Sinza-Mori, Dar, juzi Afande alisema hadi kufikia hatua ya yeye kutangaza kuwa ameachana na mama Tunda ambaye amedumu naye kama mume na mke kwa zaidi ya miaka 10, alikuwa akivumilia mambo mengi na mwisho kuamua kuachia ngazi.

Afande Sele akiwa na familia yake.
“Nilikuwa nikielezwa mengi kuhusu mke wangu, nilishapigiwa simu na kuambiwa mke wangu anagombaniwa na wanaume usiku klabu lakini huwa mimi siyo mtu wa kuishi kwa hisia, nilivumilia nikiamini atajirekebisha, haikuwa hivyo.
“Japo sikuwa na uthibitisho wa moja kwa moja, lakini nyumbani alikuwa siyo mtu wa kutulia, amekuwa akinizunguka hadi kwa washkaji zangu wa karibu. Kuna jamaa alichoshwa na habari hizo akanifuata na kuniambia hata kama lakini uvumilivu wangu ulizidi,” alisema Afande kwa hisia.
Akiendelea kushusha masikitiko yake mbele ya kinasa sauti cha Risasi Jumamosi, Afande alienda mbele zaidi kwa kusema mbali na mkewe huyo kumsaliti kwa wanaume tofauti wakiwema marafiki zake, ilifika wakati mama Tunda akawa anachukua fedha ndani na kwenda kutumia na wanaume.
Alisema alitumia mwanya wa mkali huyo wa mashairi anapokuwa amesafiri katika shoo mbalimbali na kuachiwa fedha za matumizi pamoja na ujenzi wa nyumba yao mpya, kutanulia.
“We acha tu, yaani fedha za matumizi, ujenzi nilikuwa namuachia lakini cha kusikitisha ni kwamba alizitumia kutanulia, jambo ambalo nililizidi kunitia umaskini na machungu ukizingatia jamii inaniheshimu kama msanii, mbaya zaidi wananchi wamenitaka nigombee ubunge Morogoro Mjini,” alisema Afande.
Akizidi kushusha ‘vesi’, Afande alitiririka kuwa kuna wakati aliwahi kupewa taarifa na rafiki yake mwingine aishie Kurasini jijini Dar ambaye alilamika juu ya mkewe kufika kwa jamaa huyo na kuazima fedha bila kuzilipa.
Kwenye aya nyingine, mkali huyo alisema anakumbuka jinsi alivyoishi na familia yake, mkewe, wanaye Tunda na Ahsante Sanaa lakini hana jinsi kwani ameona bora kuachana kwani umri wake una mruhusu kuoa mke mwingine siku ikitokea.
“Nakumbuka maisha kidogo ya furaha na familia, mama Tunda atabaki kuwa mama wa watoto wangu lakini kamwe hawezi kurudi kwangu kwani itakuwa ni aibu juu ya aibu,” alisema.
Afande aliachana na mama Tunda mwishoni mwa mwaka jana alipotimba jijini Dar katika shughuli zake za kikazi na kumuachia mkewe fedha za ujenzi lakini aliporejea nyumbani Morogoro, alikuta mzazi mwenzake huyo ameondoka nyumbani na kuacha funguo, kila alipompigia simu hakupokea.
Alipoulizwa kuhusiana na shutuma zilizoporomoshwa na Afande, mama Tunda alitiririka:
“Alinipa Sh. milioni 3 za shoo tu, tukanunua vifaa vya ujenzi lakini siyo kwamba nilitanua na wanaume, tena kama ni kumfumania, mimi ndiye nilimkuta na mwanamke alitoka naye Fiesta Dodoma, sikutaka tu kumsema, hizo taarifa anazusha tu.
“Kwanza kuna mambo mengi tu amenifanyia, alikuwa mlevi kwani hadi wazazi wangu walikuwa wakinishangaa sana, sasa na mimi nikaona bora niachane naye,” alisema mama Tunda.

AMANDA NA GONJWA LISILOELEWEKA

Stori: Gladness Mallya
STAA wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’ amepatwa na ugonjwa wa ajabu  ambao haujulikani.
Staa wa sinema za Kibongo, Tamrina Posh ‘Amanda’.
Katika mazungumzo na paparazi wetu, Amanda alisema: “Naumwa sana na nimechukua vipimo vingi ikiwemo malaria na presha pale Agha Khan (hospitali) lakini hakijagundulika chochote ingawa mwili wote unauma.”

WEMA SEPETU"NAPENDA WANAUME WEUSI NA NI KWELI NIPO NA DIAMOND"


Mwanadada Wema Sepetu ambaye pia aliwahi kuwa Miss Tanzania 2006 ambaye kwa sasa anaendesha kampuni yake binafsi iitwayo Endless Fame inayojishughulisha zaidi na utengenezaji wa Filamu mbalimbali.

Kupitia kipindi cha Leo tena February 28 Wema Sepetu amekubali kutaja sifa za mwanaume anayempenda kuwa na mvuto kwake,swali lililoulizwa na Watangazaji wa kipindi hicho ni kuhusu mwanaume wa sifa gani anayedhani anaweza kuolewa nae ambapo Wema alijibu “Kuolewa sio shida je huyo mwanaume nampenda,maana naweza kuja kuchumbiwa lakini nisimpende”


“Mimi nampenda Mwanaume mweusi,wanaume weupe sio kwamba sijawahi kuwa nao lakini nakuwa sina mzuka nao”.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Diamond amekiri kwa kusema’Kweli niko na Nasib - Diamond na nadhani muda huu kutakua na utulivu ndani yake,ule utoto tuliokua tunafanya nadhani ulikua utoto na imekua Power Couple toka mwaka 2010 kwa hiyo tuna ni miaka 4 sasa,kwa sasa tumeamua kuwa serious’.

Habari kwa Hisani ya Millard Ayo

Wema Sepetu pia kaandamana na Ant Ezekiel kwenye interview ya kipindi hicho kinachorushwa na Clouds Fm.

WASTARA: NINAHITAJI KUPUMZIKA, KUJIFUNGIA


Stori: Brighton Masalu
STAA wa kike mwenye uwezo wa kucheza na hisia kwenye filamu za Kibongo, Wastara Juma, amesema kwa sasa anahitaji muda mwingi wa kupumzika kutokana na misukusuko mingi iliyomkumba siku za hivi karibuni.
Wastara Juma.

Akiteta na paparazi wetu kwa sauti ya chini na ya upole alisema: “Nahitaji muda mwingi wa kupumzika jamani, kuna mambo yameniondoa kabisa kwenye ‘mudi’ ya kawaida hivyo natumia muda mwingi kuwa peke yangu.”