POOL PARTY

POOL PARTY

Tuesday, July 23, 2013

Video clip: DJ PQ AKIFANYA YAKE KWENYE BBA HOUSE.


CHEKI NISHA ALIVYOFUTURISHA WATU KIBAO NYUMBANI KWAKE! CHEKI HAPA!!!!!

Muigizaji Salma Jabu Maarufu kama Nisha ametoa mwaliko kwa marafiki zake wote na mashabiki wake wote kuungana naye nyumbani kwake maeneo ya kijtonyama kwa ajili ya kushirki naye kwenye futari maalumu aliyoindaa kwa ajili yao
Katika taarifa aliyoitoa kupitia mtandao wa
kijamii wa instagram, Nisha amesema tofauti na watu wengi walivyokuwa wakisema kuwa futari hii ni maalum kwa marafiki zake tuu si kweli kwani ameandaa kwa mtu yoyote anayetaka kujumuika naye siku ya kesho tarehe 21/07/2013.
Mwaliko wake kwa watu wote unasema….
"Naomba nichukue fursa hii kumkaribisha kila mmoja ambae atapenda kujumuika nasi siku ya kesho,ndugu yangu,shabiki wangu,rafiki yangu na kila mtu.ahsante sana .. nawapenda sana,Tujumuike pamoja kwa ajili ya Allah subhannallah wataallah RAMADHAN KAREEM..

ILE KAULI YA KWAMBA DIAMOND PLATNUMZ NI FREEMASON SASA INANUKIA NUKIA! CHEKI ANAVYOTABIRI KIFO CHAKE!!!!

Msanii anayefanya vizuri sana kwa sasa Afrika mashariki Nasib Abdul aka Diamond Platnumz amezungumza maneno mazito aliyokiri huwa yanamtoa machozi, ni mambo yanayohusiana na ‘kifo chake’
Dakika chache zilizopita hit maker huyo wa ‘Kesho’ ame post picha Instagram yenyesura yake na maswali yanayouliza nini kitatokea baada ya kifo chake. Tazama picha hiyo inazungumza yenyewe
Picha hiyo ilisindikizwa na caption hii
“One of my songs,always gets me crying whenever I listen to it, how I wish u would hear it, but then again I have no clue as to when I will release it… #WCB”

Platnumz amekaa kimya bila kutoa wimbo mpya kwa muda sasa, je unahisi kuna uwezekano ‘KAMA NIKIFA KESHO’ ukawa ndio wimbo mpya anaotegemea kuachia hivi karibuni? Tusubiri tuone!

BIRTHDAY PARTY YA KAJALA NA B12 ILIYOFANYIKA NYUMBANI KWA WEMA SEPETU





































AGOSTI 13 MWAKA HUU NDIO TAREHE YA QUEEN VIDEO MAARUFU TANZANIA KUPANDISHWA KIZIMBANI KWA TUHUMA YA KUKAMATWA NA MADAWA YA KULEVYA! SOMA HAPA



Hatima ya msanii anayeshiriki katika video za wasanii wa muziki wa bongo fleva, Agnes Jerald 'Masogange' na mwenzake Melisa Edward, waliokamatwa Afrika Kusini na dawa za kulevya kesi yao inatarajiwa kusomwa tena tarehe 13 Agosti mwaka huu nchini humo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa aliweka wazi kuwa wanadada hao wawili tayari walishapandishwa kizimbani wiki iliyopita.

Alisema kuwa kutokana na ushahidi kutokukamilika ndiyo sababu ya akinadada hao kusubiri kupanda kizimbani tena tarehe 13 ya mwezi ujao.

Kamanda Nzowa aliweka wazi kuwa nchi zote mbili zinashirikiana kwa ajili ya kufanya upelelezi wa jambo hilo: "Nchi zote mbili tunategemeana kwa upelelezi, hivyo sisi huku tunafanya wa kwetu na wao wanafanya wa kwao mwishoni tunaulizana tulipofikia hivyo ndivyo tunavyofanya kazi," alisema Nzowa.

Wadada hao ambao walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakitokea Tanzania, walikutwa na dawa za kutengenezea dawa za kulevya, ambazo hazina matumizi nchini,  zenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni sita.

AMA KWELI UTENGENEZAJI WA MOVIE HAPA TZ UMEKUA! HEBU MCHEKI MLIMBWENDE HUYU KUTOKA BONGO MOVIE AJIFUA KWA MAANDALIZI YA MOVIE MPYA! KISASA ZAIDI!!!!

 MSANII kutoka Bongo Movie mwana dada ''Nisha bebee'' Ambaye ni mmoja kati ya wasanii wa kike wanao miliki kampuni ya movie hapa nchini,
Akiwa mazoezini anasema baada ya kufanya vizuri kwenye pusi na paku na tikisa sasa wadau wake wakae mkao wa kula kuipokea filamu mpya hivi karibuni ataingia kambini. aliongea na Masai Nyotambofu Blog leo asubuhi 23/JULY/2013.

Monday, July 22, 2013

NI KWELI KWAMBA LINNAH KABAKWA?

 


Mrembo na mwanamuziki wa kike nchini, Linah Sanga amezikanusha ripoti zilizosambazwa leo kuwa amebakwa na rapper Kimbunga na kudai kuwa ameshangazwa mno na taarifa hizo.
CONTINUE Taarifa hizo zimeanza kusambazwa leo mchana baada ya akaunti ya Facebook inayoonekana kuwa ya rapper Kalapina yenye jina ‘KalApina Kikosi Cha Mizinga’ kuandika:
 
“Mtoto kimbunga amechamba ana leta usela mavi mambo ya kizamani hivi yupo chini ya ulinzi osterbay police kwa kosa la kumbaka msanii lina.”


Mwandishi wetu amezungumza na Linah ambaye amesema amepigiwa simu na watu wengi wa karibu kumuuliza suala hilo wakiwemo, Barnaba, Ditto, Amini na mtangazaji wa Clouds FM, Soudy Brown.

 
Amesema Soudy alimwambia kuwa ameziona taarifa hizo kwenye Facebook kwenye akaunti ya Kalapina.
“Sasa nikasema Kalapina ameandika hivi, kwasababu sijaingia mwenyewe kuangalia chochote. 

"Sikutaka kujipa stress kwasababu kuna kazi nafanya nisije nikaharibu kazi kwahiyo nikaona vitu vingine kama hivi ni vya kupotezea tu lakini sio vizuri kabisa yaani.

 "Kiukweli sijapenda, yaani bora mtu anizushie kitu kingine chochote lakini si suala kama hilo hapo, si suala zuri,” amesema Linah.
 
Amesema jana usiku alitoka na mpenzi wake kwenda kwenye sinema na wakarejea nyumbani salama.


“Sasa sielewi huko kubakwa nimebakwa saa ngapi na nilikuwa na boyfriend wangu labda yeye ndio kanibaka! Maana mtu wanayeniambia amenibaka Kimbunga, huyo Kimbunga hata simjui, namskia tu.
 
Nashindwa kuelewa, kwanini mtu azushe kiu kama hicho yaani ndo nataka kujua source ni nini. Niko fine yaani, kwasababu naelewa ‘it’s not true, lakini nafikiria huyo mtu mpaka kaamua kunifanyia kitu kama hicho, nimemkosea nini au kuna kitu gani, yaani hicho ndio kinaniumiza kichwa.