POOL PARTY

POOL PARTY

Wednesday, December 17, 2014

MSIMU WA SIKUKUU DAR LIVE, WASANII WAELEZEA WALIVYOJIPANGA KUPOROMOSHA BURUDANI KALI

Mfalme wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live. …
Mfalme wa Muziki wa Taarab nchini, Mzee Yusuf (wa pili kushoto) akielezea kwa wanahabari (hawapo pichani) alivyojipanga kuanguasha shoo ya nguvu katika Tamasha la Wafalme Sikukuu ya Xmas Dar Live. 
Meneja wa Mashauzi Classic, Ismail Rashid 'Suma Ragar' akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi walivyojipanga kutoa burudani katika msimu wa Xmas Dar Live wakati wa mkutano na wanahabari hao uliofanyika leo kwenye Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana jijini Dar . Kushoto ni Mratibu wa tamasha hilo, Benjamin Mwanambuu, Mkurugenzi Bendi ya Extra Bongo, Ali Choki (wa pili kushoto), Mzee Yusuf (wa pili kulia) na Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (wa kw nza kulia).
Damian Raphael 'MC Dalada Kikombe' kutoka Kundi la Masai Worriors (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu makamuzi watakayoyafanya Dar Live katika msimu huu wa sikukuu.
KAMPUNI ya Dar Live kwa mara nyingine imetoa ratiba kamili ya burudani katika msimu huu wa kufungia mwaka 2014 na kuukaribisha mwaka 2015.
Usiku wa Wafalme
Kwa mara nyingine shoo bab’kubwa ambayo ni habari ya mjini kwa sasa ijulikanayo kama Usiku wa Wafalme itagongwa ndani ya ukumbi huo pekee kwa burudani, Desemba 25 ‘Sikukuu ya Krismasi’ ambapo mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ atagonga nyimbo zake zote kali siku hiyo.
Diamond ambaye ni mshindi wa tuzo tatu kutoka Channel O zijulikanazo kama Channel O Africa Music Video Awards (CHOAMVA), siku hiyo atatinga na tuzo zake zote hizo ikiwa ni kuwapa shukrani mashabiki wake wote kwa sapoti waliyoitoa huku akipiga nao picha kwenye ‘red carpet’ na kuongea nao mawili-matatu.
Mashabiki pia watapata nafasi ya kumshuhudia Diamond kwa mara ya kwanza akipiga nyimbo zaidi ya 20 jukwaani pasipo kusimama huku akiwatambulisha madensa wapya sambamba na kupiga pia na nyimbo zake zote ambazo zilishawahi kuachiwa na hazijawahi kuisha mpaka mwisho.
Kwa upande wa muziki wa Pwani, usiku huo utafunikwa pia na Mfalme Mzee Yusuf ambaye siku hiyo ataungana na kundi lake la Jahazi Modern Taarab katika kuwaonjesha mashabiki ngoma zao zote zilizopo katika albamu yao mpya ya Chozi la Mama huku wakifunga mwaka na ngoma ambayo ni habari nyingine kwa sasa ya Mahaba Niue.
Mashabiki watakaofika usiku huo pia watapata bahati ya kushuhudia mshindi wa shindano la kumtafuta mwanaume mwenye mvuto kutoka Gazeti la Ijumaa lijulikanalo kama Ijumaa Sexiest Bachelor ambapo mpaka sasa wamebaki washiriki watatu, Yusuph Mlela, Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba.
Mapema kuanzia asubuhi hadi jioni kutakuwa na burudani kwa watoto ambapo watoto wote watakaofika watapata bahati ya kucheza michezo kibao kama vile kubembea, kuteleza, kuogelea na mingine mingi huku kundi la sarakasi la Masai Worriors likiwapagawisha kwa kutoa michezo kibao ya sarakasi , mazingaombwe sambamba na kumwaga zawadi kwa kila mtoto.

AISHA MADINDA AFARIKI DUNIA!

 
 
Aisha Madinda - enzi za uhai wake
Aisha Madinda - enzi za uhai wake alipokuwa stejini
Aisha Madinda - enzi za uhai wake akitambulishwa na Ally Choki alipojiunga na Extra Bongo
ALIYEKUWA mnenguaji na mwimbaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda amefariki dunia hivi punde jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa ASET, Asha Baraka amethibitisha kutokea kifo hicho na kuongeza kuwa mwili wa marehemu kwa sasa umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala, Dar.
Kujua matukio na stori mbali mbali alizowahi kupitia msanii huyu maarufu Bongo na kuripotiwa na mtandao huu, nenda hapa: STORI ZA AISHA MADINDA
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMEN!

Monday, December 15, 2014

Ujumbe Wa Happiness Watimanywa Baada Ya Miss World 2014.



Mwakilishi wa Miss World 2014 ametulita pamoja kama nchi kwenye kumpa ushirikiano katika kupiga kura ili ashinde peoples choice awards na kuingia kwenye top ten ya miss world. Ingawa hatukufanikiwa kumweka namba moja Happy ameonekana mtu mwenye kujiamini na kujituma sana. Hizi ni picha zake kwenye show ya Miss World na ujumbe wake baada ya show kuisha.



Kutoka Instagram yake Happy ameandika ” Nampongeza @rolenestrauss (South Africa) kwa kuibuka mshindi Miss World 2014.
Watanzania wenzangu na marafiki kutoka mataifa mengine, tumepiga kura sana, mmeonyesha support kubwa kuliko matarajio ya wengi bahati mbaya kura hazikutosha.
Natumia nafasi hii kuwashukuru wote mmoja mmoja kwa kuniunga mkono kwa kipindi chote ambacho nilikua hapa jijini #London na tokea niliposhinda mashindano ya #MissTanzania. Nisingefika hapa bila support yako. From deep inside my heart. I thank you.

Kuanzia aliyetumia muda na pesa yake kunipigia kura, aliyeandika na kutangaza habari yangu, designers mbalimbali, familia yangu, marafiki wote, wote, wote, I thank you.
Nimejifunza vitu vingi sana kipindi chote hiki na kwakweli watanzania tumeonyesha umoja wa hali ya juu sana. Umoja wetu na udumu katika mambo yote ya kimaendeleo kwa taifa letu.

Mbarikiwe
#Happiness4MissWorld ”

Hongera Happy kwa Ulipotufikisha.

Shilole aachia ngoma yake mpya kwenye Leo Tena iitwayo Malele


Msanii wa Bongo Fleva,Shilole akiwa na mtangazaji wa kipindi cha Leo Tena,Husna Abdul wakati akiachia ngoma yake mpya iitwayo Malele.

Nywele za mwanamke zashika moto wakati akizima mshumaa siku ya birthday yake

 
Hii imetokea huko Marekani! Mwanamke mmoja Shelley Meyer amejikuta sherehe yake ya siku ya kuzaliwa ikigeuka kilio baada ya nywele zake kuteketea kwa moto wakati akizima mishumaa kwenye keki yake.

Shelley ambaye alikua akisherekea mwaka wake wa 5 tangu azaliwe haweza kumaliza vyema sherehe hiyo kwani wakati akiazimisha miaka hiyo kwa kuzima mishumaa iliyokua juu ya keki hiyo gafla nyele zake zilishika moto na kuungua.Taarifa zinaeleza kuwa mumewe ambaye ni kocha wa mpira wa miguu aliamua kumshangaza mkewe kwa kumfanyia sherehe ya kutimiza miaka50 ambapo wakati wakisherehekea mwanamke huyo alijikuta akipatwa na maswaiba hayo na kukimbizwa hospitali.

Wakati nywele zake zikiungua mtoto wake wa kike Nicki Meyer alikua akimpiga picha badala ya kumsaidia na kuandika ujumbe mfupi wa kumjulisha mama yake juu ya tukio hilo na kumpa pole kwa matatizo aliyoyapata.

Tukio kama hilo liliwahi kumpata pia msichana mdogo wa miaka 12 wakati akisherehe siku yake yakuzaliwa.

GARI LA DIAMOND LAMCHEFUA WEMA

Stori: Musa Mateja
LILE ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond’, limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.
Ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake, Nasibu Abdul ‘Diamond'.
Tukio hilo lilijidhihirisha wazi mbele ya paparazi wetu juzikati nyumbani kwa staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.
Wema Sepetu akitafakari jambo.
“Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano sitaki hata kulisikia, sijui najisikiaje hata nikiliona,” alisikika Wema.Paparazi wetu baada ya kusikia Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo, alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini analichukia ingawa ni mali yake.
“Siku hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli, inafikia kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana najikuta nalichukia gari hili,” alisema Wema.
Nasibu Abdul ‘Diamond'akipozi.
Kwenye bethidei yake iliyofanyika Septemba, mwaka huu, Wema alizawadiwa magari mawili. La kwanza lilikuwa ni BMW 545i (Sh. Milioni 56) ambalo liliibua utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan Murano (Sh. milioni 36) alilopewa na Diamond.

ROSE MUHANDO AYASUSA MAZISHI YA DADA'KE!

Stori: Dunstan Shekidele, Morogoro
Why? Mwimbaji maarufu wa nyimbo za lnjili Bongo, Rose Muhando ameshindwa kuhudhuria mazishi ya dada yake wa damu, jambo lililowakera baadhi ya ndugu, jamaa na marafiki.
Waombolezaji wakiwa msibani.
TUJIUNGE KIJIJI CHA MAGOLE
Ishu hiyo ilijiri wikiendi iliyopita nyumbani kwa wazazi wa staa huyo katika Kijiji cha Magole, Dumila wilayani Kilosa mkoani hapa ambapo dada wa tumbo moja (toka, nitoke) wa Rose aitwaye Shida Athuman Muhando alifariki dunia ghafla.
Ndugu na jamaa wa marehemu dada yake Rose Muhando wakilia kwa uchungu.
Mwandishi wetu ambaye alifika kijijini hapo, alielezwa kwamba Shida alikuwa akitibiwa katika Zahanati ya Roma iliyopo Dumila (ugonjwa haukutajwa) ambapo Rose alipewa taarifa lakini hakufika.
Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa marehemu Shida na mjomba mkubwa wa marehemu, Mohamed Seif Matambo, Rose alipewa taarifa juu ya kifo hicho lakini hadi mazishi yanafanyika hakufika na alipopigiwa simu, muda wote iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa kumpa pole hakujibu.
Marehemu dada wa Rose Muhando, Shida Athuman Muhando enzi za uhai wake.
“Rose anayejifanya ana fedha, hataki hata kuzika ndugu zake,” alifoka mmoja wa vijana waliohudhuria mazishi hayo aliyejulikana kwa jina moja la Kesi na kuongeza:
“Rose ni dada yetu wa damu, juzikati alifariki dunia Semeni (mtoto wa dada wa Rose) hakuja kuzika, sasa amefariki dunia Shida.
ROSE ASIKITIKA
“Tulimpigia simu akasikitika sana, akasema anakuja. Siku mbili mfululizo tumempigia na kumtumia ujumbe mfupi (SMS) hadi sasa ni saa 10:00 jioni. “Anajua kabisa kwamba tunamsubiri yeye kwa kuwa ndiye aliyeachiwa familia lakini kinachoonekana ametususia. Tunasikia yupo Dar. Tumeona muda unayoyoma tukawaambia mashehe tumpumzishe marehemu kwani mtu mwenyewe hatujui kama atakuja.
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za lnjili Bongo, Rose Muhando.
KUMBE NI MKRISTO PEKEE
“Katika familia hii, yeye pekee ndiye Mkristo hivyo kinachoonekana anataka kujitenga na sisi kwani alianza muda mrefu.
ROSE VIPI?
Ijumaa Wikienda lilimpigia simu Rose kwa lengo la kutaka kujua sababu zilizomfanya ashindwe kwenda kwenye msiba wa dada yake lakini simu iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa SMS za kumwaga hakujibu.