POOL PARTY
Monday, December 15, 2014
MISS TZ AFARIKI GHAFLA
KWELI kifo hakina huruma jamani! Mshiriki wa Miss Tanzania 2013 akitokea Miss Ilala, Martha Gewe, mkazi wa Tabata Segerea, Dar amefariki dunia baada ya kuugua ghafla, Ijumaa Wikienda linakupa zaidi.
AFYA YAKE SIKU ZA NYUMA
Habari zaidi zinasema kuwa mrembo huyo hakuwa akisumbuliwa na ugonjwa wowote huko nyuma na alionekana mwenye afya njema huku mipango yake ikiwa imelenga jinsi atakavyoisherehekea Sikukuu ya Krismasi.
“Lakini Jumatano iliyopita alianza kuumwa, alisema anahisi homa ambayo baadaye ikabainika ni malaria.
“Tulimpeleka Amana, akalazwa kwa siku tatu tu, leo (Ijumaa) akafariki
dunia. Madaktari wamesema ile malaria kukimbilia kichwani ndiyo
tatizo,” alisema ndugu mmoja wa marehemu huyo kwa sharti la kutochorwa
jina gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa familia ya mzee Gewe.
WALICHOSEMA MADAKTARI
Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda kichwani.
“Mpaka sasa bado malaria ni tishio, inaua watu wengi sana. Kwa
malaria kupanda kichwani ni hatari zaidi kwani mgonjwa anaweza kupoteza
maisha ndani ya muda mfupi sana.Ijumaa Wikienda lilifanikiwa kuzungumza na madaktari wawili wa Hospitali ya Amana jijini Dar kuhusu ugonjwa wa malaria kupanda kichwani.
“Kikubwa watu wazingatie kuwa mbali na mazingira hatarishi kwa ugonjwa huo na wajichunge kuumwa na mbu ambao ndiyo wana-oeneza ugonjwa huo,” alisema daktari mmoja.
MAMISI WENZAKE NI MACHOZI
Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini kilimpata mwenzao huyo!
“Kwa kweli nilipopata taarifa za kifo cha Martha sikuamini mara moja
kwa vile sijawahi kusikia akiumwa au hata kwamba alilazwa kwa muda
mrefu.Kufuatia taarifa za kifo hicho, mamisi wenzake walipigwa na mshangao, wengine wakiuliza nini kilimpata mwenzao huyo!
“Kifo chake kimeniumiza sana, sijui hata nisemeje jamani, kweli kifo hakina huruma,” alisema Miss Ilala 2013, Dorice Mollel huku akilia.
Mrembo mmoja ambaye hakutaja jina lake alisikika akisema: “Yaani Happiness (Watimanywa) yuko Uingereza kusaka taji mwenzake anapoteza maisha ghafla hapa nyumbani Tanzania! Inauma sana kwa kweli.”
Warembo wengine walioshiriki msiba wa Martha nyumbani kwao, Tabata, Dar walishindwa kujizuia na kujikuta wakibubujikwa machozi muda wote kiasi cha kushindwa kuongea na mwandishi wa gazeti hili.
HISTORIA YA MARTHA KATIKA UMISI
Mwaka jana, Martha alishiriki shindano la kumsaka Redd’s Miss Ukonga lililofanyika katika Ukumbi wa Wenge Garden, Ukonga Mombasa jijini Dar.
Katika kinyang’anyiro hicho, Martha
aliibuka kidedea kwa kuvalishwa taji hivyo kupata tiketi ya kwenda
kushiriki Miss Ilala 2013 kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee Tower, Dar
ambapo mshindi alikuwa Dorice.
Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
Watimanywa usiku wa kuamkia leo, kule jijini London, Uingereza alifurukuta kugombea Taji la Miss World!Marehemu alipata nafasi ya kuvuka Miss Ilala na kushiriki Redd’s Miss Tanzania 2013 chini ya Hashim Lundenga ‘Anko’ na kufanikiwa kuwa miongoni mwa Kumi Bora huku Happiness Watimanywa akiibuka mshindi.
MAZISHI YA MARTHA
Marehemu Martha alizikwa Jumamosi iliyopita kwenye makaburi ya nyumbani kwao, Tabata Segerea jijini Dar es Salaam huku msiba huo ukihudhuriwa pia na warembo mbalimbali ambao wamewahi kuvaa mataji nchini.
UNGANA NASI KATIKA FACEBOOK, TWITTER , INSTAGRAM
VITUO VITATU VYA WATOTO WENYE UHITAJI MAALUM VYAPOKEA ZAWADI ZA KRISMASI KUTOKA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF

Kulia
ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick
Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu
Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa
ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga zawadi za Sikukuu
ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.
Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF
kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo
la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo
katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba
wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine
wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi
kabisa katika mfuko huo.…

Kulia
ni Afisa Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga Erick
Chinimbaga na wa kwanza kushoto ni Afisa Fedha kutoka PSPF Makao Makuu
Samweli Haule wakiwakabidhi zawadi za Krismasi watoto wenye ulemavu wa
ngozi katika kituo cha Buhangija kilichopo Shinyanga zawadi za Sikukuu
ya Krismasi hapa watoto wenzao wakipokea zawadi hizo kwa niaba.
Akikabidhi Msaada huo Afisa Fedha wa PSPF
kutoka Makao Makuu alisema kwamba Mfuko wa Pensheni wa PSPF unalo lengo
la kuwasaidia watoto wenye Uhitaji Maalum ili nao waweze kujisikia wapo
katika jamii kama watoto wengine na kwamba kuwa hapo sio ndio kwamba
wametengwa, alisisitiza kuwa Hata watakapo kuwa wakubwa wengine
wataikuta PSPF na watakuwa wanachama na wengine watakuja kufanya kazi
kabisa katika mfuko huo.
Mlezi
wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Buloma Foundation kilichopo
Picha ya Ndege Kibaha Bi Simphania Aidan wa kwanza kushoto akipokea
Zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa niaba ya Msimamizi na Mwenye kituo
hicho Bi.Fransisca Kyando Kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF , wa katikati
ni Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri Mugaka na wa kwanza kulia ni
Afisa Mahusiano wa PSPF Coleta Mnyamani.
Watoto wakipokea zawadi za Krismasi kwa Niaba ya wenzao.
Picha
ya pamoja ya Ma Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF na watoto pamoja na
Mlezi wao baada ya kupokea zawadi hizo kwa ajili ya Sikukuu ya Krismasi.

Afisa
Mfawidhi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF Mkoa wa Shinyanga wa pili
kushoto Erick Chinimbaga akimkabidhi zawadi Mmoja wa walezi wa watoto
hao bwana Revocatus Robert wa kwanza Kulia zawadi za Sikukuu ya
Krismasi kwa Wasichana waliotoka katika Mazingira magumu wanaolelewa na
Kituo cha Agape Mkoani shinyanga, wasichana hao walipata zawadi za
Mafuta, Mbuzi, Mchele, Sabuni,Sukari pamoja na vitu.
Akikabidhi Msaada huo Meneja wa PSPF Mkoa wa Pwani Msafiri
Mugaka alisema kuwa PSPF inatoa zawadi za Sikukuu ya Krismasi kwa watoto
yatima ili nao washerekee vizuri na wasijisikie vibaya , aliongeza kuwa
pamoja na PSPF kuwa na wanachama watu wazima lakini pia inafanya hivyo
kwa watoto ili waanze kuijua PSPF wakiwa wadogo na wakiwa watu wazima
waje kuikumbuka na kujiunga na Mfuko huo Bora wa Pensheni na hata kuja
kufanya kazi katika Mfuko huo.
Nae Afisa Mahusiano wa PSPF kutoka Makao Makuu Coleta Mnyamani
Aliongeza neno kuwa Watoto yatima ni kama watoto wengine ambao
wanahitaji kupata huduma na malezi Bora kama watoto wengine wenye wazazi
au wanaolelewa bila shida yotote, alimalizia kwa kusema kuwa PSPF ipo
pamoja na watoto hao wenye uhitaji na itaendelea kuwasaidia
ROLENE STRAUSS WA AFRIKA KUSINI ASHINDA TAJI LA MISS WORLD 2014
Miss World 2014, Rolene Strauss wa Afrika Kusini.…
Miss World 2014, Rolene Strauss wa Afrika Kusini.
Miss World 2014, Rolene Strauss akipozi na mshindi wa pili Edina Kulcsar wa Hungary na Elizabeth Safrit wa Marekani aliyekuwa mshindi wa tatu.
Washereheshaji wa shindano hilo Miss World 2013, Megan Young akiwa na mtangazaji wa Tim Vincent.
Miss Mongolia Battsetseg Turbat akifanya yake stejini.
Miss Bolivia, Andrea Forfori Aguilera akifanya yake stejini.
Miss Gabon, Miss Ethiopia, Miss Curacao na Miss Chad stejini.
Rolene
Strauss wa Afrika Kusini ameshinda taji la Miss World 2014 jijini London
usiku huu, Edina Kulcsar wa Hungary akishika nafasi ya pili na
Elizabeth Safrit wa Marekani akichukua nafasi ya tatu.Rolene ana umri wa miaka 22, ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa shahada ya udaktari na anapendelea kucheza michezo ya golf, netiboli, kuendesha baiskeli na kujisomea vitabu vya burudani na elimu.
Washindi walioingia Tano Bora mwaka huu walikuwa kutoka Uingereza, Marekani, Hungary, Australia na Afrika Kusini.
HAUSIGELI ALIYEMTESA MTOTO UGANDA AHUKUMIWA MIAKA 4 JELA
Jolly Tumuhirwe (22).
HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda,
amehukumiwa kwenda jela miaka minne katika mahakama moja nchini humo.
Jolly Tumuhirwe wakati akimtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe (22) aliiambia mahakama kuwa anajutia
kile alichokifanya na anaomba msamaha kwa familia na jamii nzima.Amehukumiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella…
Jolly Tumuhirwe (22).
HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda,
amehukumiwa kwenda jela miaka minne katika mahakama moja nchini humo.
Jolly Tumuhirwe wakati akimtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.
Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe (22) aliiambia mahakama kuwa anajutia
kile alichokifanya na anaomba msamaha kwa familia na jamii nzima.Amehukumiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella mwenye miezi 18.
MTU MWENYE SILAHA AZIDI KUWASHIKILIA MATEKA KWENYE MGAHAWA JIJINI SYDNEY
Polisi wakimpokea mmoja wa mateka kutoka katika mgahawa wa Lindt jijini Sydney.
MTU mmoja mwenye silaha bado anaendelea kuwashikilia wafanyakazi na
wateja katika mgahawa wa Lindt uliopo jijini Sydney nchini Australia.
Mateka ndani ya mgahawa huo wakiwa wameshika bendera yenye maandishi ya Kiarabu.
Baadhi ya watu ndani ya jengo hilo wameonekana kupitia madirisha wakiwa wamebeba bendera nyeusi zenye maneno ya…
Polisi wakimpokea mmoja wa mateka kutoka katika mgahawa wa Lindt jijini Sydney.
MTU mmoja mwenye silaha bado anaendelea kuwashikilia wafanyakazi na
wateja katika mgahawa wa Lindt uliopo jijini Sydney nchini Australia.
Mateka ndani ya mgahawa huo wakiwa wameshika bendera yenye maandishi ya Kiarabu.
Baadhi ya watu ndani ya jengo hilo wameonekana kupitia madirisha wakiwa wamebeba bendera nyeusi zenye maneno ya Kiarabu.
Ulinzi mkali nje ya mgahawa.
Watu watano wameonekana wakikimbia kutoka katika jengo hilo la
mgahawa japo mpaka sasa bado haijafahamika ni mateka wangapi wapo ndani.Askari polisi waliozingira eneo lote la mgahawa huo wameeleza kuwa tayari wameanza kufanya mazungumzo na mtekaji huyo aliye ndani ya jengo.
Baadhi ya mitaa ikiwa imefungwa.
Mpaka sasa bado haijafahamika sababu za mtu huyo kuwateka watu ndani ya mgahawa huo.
Subscribe to:
Posts (Atom)