POOL PARTY
Monday, December 15, 2014
MWANAMUZIKI MKONGWE, SHEM IBRAHIM KARENGA HATUNAYE TENA
Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI mkongwe mwenye umahiri wa kuimba na kucharaza gitaa
kiongozi la Solo, Shem Ibrahim Karenga amefariki dunia leo akiwa katika
Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.Wengi wanamfahamu Shem Karenga kupitia tungo zake mbalimbali zilizochangia kumpa umarufu, alizozifyatua akiwa na bendi hizi na zile, kama vile ‘Tucheze Segere’, ‘Muna’, ‘Kila jambo’ na ‘Mbelaombe’.…
Shem Ibrahim Karenga enzi za uhai wake.
MWANAMUZIKI mkongwe mwenye umahiri wa kuimba na kucharaza gitaa
kiongozi la Solo, Shem Ibrahim Karenga amefariki dunia leo akiwa katika
Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam alipokuwa akitibiwa.Wengi wanamfahamu Shem Karenga kupitia tungo zake mbalimbali zilizochangia kumpa umarufu, alizozifyatua akiwa na bendi hizi na zile, kama vile ‘Tucheze Segere’, ‘Muna’, ‘Kila jambo’ na ‘Mbelaombe’.
Shem Karenga alizaliwa mwaka 1950, Bangwe, Kigoma na kupata elimu ya msingi katika shule ya kimishionari ya Kihezya kuanzia mwaka 1957 hadi mwaka 1964.
Mwaka 1964 alijiunga na bendi ya Lake Tanganyika Jazz ambayo maskani yake yalikuwa mjini Kigoma.
Mwaka 1972, aliitwa kwenye bendi ya Tabora Jazz kama mwanamuziki mwenye kipaji cha utunzi, mwimbaji na mpigaji wa gitaa la Solo.
Mwaka 1983 alijiengua kutoka Tabora Jazz na kusimama kabisa kujihusisha na muziki, ambako kilichofuatia ilikuwa ni kifo cha bendi hiyo.
Mwaka 1990 aliondoka Tabora na kutua jijini Dar es Salaam.
Mwaka 1990 alijiunga na MK Beats.
Mwaka 1995, MK Beats ilisambaratika, ambako mwaka uliofuata, yaani 1996 alianzisha bendi ya Tabora Jazz Star kwa kushirikiana na Ibrahim Didi.
Mpaka mauti yanamfika, Shem Karenga Mkurugenzi Msaidizi katika Bendi ya Tabora Jazz Star ambapo Mkurugenzi Mkuu ni Ibrahim Didi.
Kwa mujibu wa familia ya marehemu, Shem Karenga anatarajiwa kuzikwa kesho.
MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, AMEN
Saturday, December 13, 2014
Diamond na Dimpoz kuwania tuzo za HMA 2015

Ommy Dimpoz na Diamond wakipeana mkono wa kheri
Nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Diamond Platinum na Ommy Dimpoz wametajwa kuwania tuzo za muziki za nchini Uganda ziitwazo HiPipo Music Awards (HMA) 2015 zinazotarajiwa kutolewa rasmi February 07, 2015.
Diamond na Dimpoz watachuana katika kipengele kimoja cha ‘East Africa Super Hit’ kupitia nymbo zao Ndagushima na Number One original.
Katika kipengele hicho wakali hao watachuana na Sauti Sol, Jaguar, Eddy Kenzo, Baramushaka, Urban Boys na Bebe Cool.
Aidha, hatua hiyo inaonesha jinsi muziki wa Bongo flava unavyoendelea kufanya vizuri katika soko la muziki la kimataifa na jinsi unavyokubalika kwa kasi kubwa.
Monday, December 1, 2014
Ommy Dimpoz kutoa laki 5 kila wiki kwa wiki nne
Naamini utakuwa umeshaiona video mpya ya Ommy Dimpoz "Tupogo Remix"
ambayo imetoka leo sio? sasa Ommy ameamua kutoa laki 5 kila wiki.
Kuanzia jumatatu ijayo kupitia account zake za mitandao ya kijamii facebook
titwer na instagram @ommydimpoz atakua anaendesha shindano la kucheza wimbo huo, shindano alilolipa jina "Lima na Tupogo" ambapo kila mwisho wa wiki mshindi
atazawadiwa mtonyo laki 5 cash kutoka mfukoni kwa Ommy dimpoz.
Lima na tupogo ni moja kati ya vionjo kwenye Tupogo,
sasa kwasababu mafans wetu wanatuweka hapa na wanatufanya tuwe hapa na
wanatupa nguvu ya kufanya kazi zaidi kwahiyo nimeona hii wakati nimetoa
hii video ya tupogo, na kama kuwataka radhi hizi kwasababu uanajua
tupogo ni video ambayo ingetakiwa kutoka mda mrefu ndio maana nikaamua
nifanye remix na niitolee video, ambayo itakuwa ni kama bonus track
katika album yangu ambayo itatoka siku ya Valentines.....
Lima
na Tupogo ni style ambayo nimewapa nafasi mashabiki wa PKP kutumia
nafasi hii kulima lima lima lima, wanakuwa wanalima halafu mshindi kwa
kila wiki anaondoka na laki tano na tutakuwa na wiki nne,.....Ili
kushiriki kutakuwa na hashtag ya Lima na Tupogo ambayo
tutakuwa tunaweka clip kwenye acc yangu ya instagram facebook na twitter
kwahiyo tutakuwa tunafanya kwa kupitia social network kui-promote hiyo Lima na Tupogo na wengine kama wataweza ku-upload youtube
Diamond kurecord tena audio, video na wasanii wakubwa Africa
Mwanzoni mwa
mwaka huu msanii Diamond Platnumz aliiwakilisha Tanzania katika kampeni
iliyokuwa ikihamasisha kilimo (One Campaign) na kufanya wimbo pamoja na
video na wasanii wakubwa Africa.
Diamond
amepata nafasi hiyo kwa mara ya pili ya kufanya kazi na One Campaign na
safari hii anaungana tena na wasanii wengine kutoka Africa kwa ajili ya
kutengeneza wimbo unaopiga vita ugonjwa wa Ebola
"Kwa taarifa ambazo nimezipata tutatumia beat ya we are the world, tutaimba na kushoot video" amesema Diamond
Licha yakuchaguliwa kuwepo katika kugombani tuzo za hannel O, zitakazofanyika weekend hii Diamnd pia amepata shavu
la kutoa tuzo mojawapo
"Channel O pia ntatoa Tunzo pale sa subiri uone vingereza vyangu vya kushoto kulia pale wakati natoa tunzo
Baada ya colabo na T.I, Psquare waja na video hii mpya
wasanii wawili wakali Africa wanaounda kundi la Psquare kutoka Nigeria wamekuja na video ya pili mpya "Shekini" kutoka kwenye album yao ya 6 iliyoingia sokoni hivi karibuni "Double Trouble"
Kama
unaangalia sana Tv za kimataifa utagundua kuwa video ya Psquare feat T.I
"Eje ajo" inafanya vizuri sana na inachezwa kila baada ya muda lakini
ukiangalia video hii utagundua kuwa mivunjo ya ndani imeitendea haki
ngoma hiyo ambapo wanaonekana wakiwa wamejumuika na dancers wadogo wenye
mivunjo ya hatari...
Subscribe to:
Posts (Atom)


