Wakati Kenya, Rwanda na Uganda zimeunda umoja unaoitwa `Umoja wa Walio Tayari’ , Tanzania, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) nazo zimeanzisha ushirikiano baina yao.
Katika
siku za karibuni kumekuwa na mtikisiko ndani ya Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) baada ya Tanzania na Burundi kutengwa na wenzao wa
Kenya, Rwanda na Uganda katika baadhi ya masuala muhimu ya ushirikiano
hasa wa kiuchumi.
Tanzania,
Burundi na DRC nazo zimekutana ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Waziri
wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta ambaye aliliambia Bunge
lililopita kuwa Tanzania inafikiria kushirikiana na nchi hizo.
Mkutano wa ujirani mwema
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya mkutano wa Ujirani Mwema uliofanyika
mjini Bujumbura, Burundi jana, Sitta alisema Tanzania, Burundi na Kongo
zimekubaliana kuendeleza miundombinu ya barabara, reli, anga na usafiri
wa maji katika Ziwa Tanganyika.
Alisema
mkutano huo ulilenga kuboresha miundombinu ya usafiri katika Ziwa
Tanganyika ambalo linaziunganisha Burundi Tanzania, DRC na Zambia.
“Pia
tumepanga kuendeleza reli ya kati kutoka eneo la Uvinza, Tanzania hadi
Msongati, Burundi na pia kuunganisha Barabara ya Manyoni - Tabora -
Kigoma kupitia Bujumbura hadi Kivu ya Kusini, DRC,” alisema Sitta.
Mkutano
huo ulihudhuriwa na Sitta pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika
Mashariki wa Burundi, Leontine Nzeyimana na Waziri wa Uchukuzi wa DRC,
Jack Lukeba.
“Pia
tulitembelea Bandari ya Kalindo iliyoko katika Ziwa Tanganyika upande
wa Burundi kwani tunataka kuboresha bandari za ziwa hilo,” alisema Sitta.
Waziri
huyo alisema Tanzania na Burundi zitaunganishwa na Barabara ya Manyoni –
Tabora - Kigoma na Barabara ya Manyovu - Mgina, Mabanda - Bujumbura
itakayounganishwa mpaka Kivu ya Kusini, DRC.
Kuhusu
usafiri wa anga, Sitta alisema nchi hizo zinaangalia uwezekano wa
kuanzisha safari za ndege za Dar es Salaam mpaka Bujumbura.